AFYA

MKUU WA WILAYA KILWA AIPA SIKU 21 MENEJIMENTI YA KAMPUNI UCHIMBAJI ISHUGHULIKIE MADAI YA WAFANYAKAZI

on

Na. Ahmad Mmow, Kilwa

Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, Christopher Ngubiagai, ameipa siku 21 kampuni ya uchimbaji na uuzaji madini ya jasi ya Kilwa Kwanza, ishugulikie madai na changamoto mbalimbali zinazo wakabili wafanyakazi wake.

Ngubiagai alitoa agizo hilo katika kijiji cha Mtandi baada ya kupokea malalamiko ya wafanyakazi na vibarua wanaofanya kazi kwenye kampuni hiyo alipokuwa anazungumza na wafanyakazi, vibarua na menejimenti ya kampuni hiyo. Alisema nchi yetu inahitaji wawekezaji, hata hivyo wawekezaji hao nilazima wazingatie sheria za nchi na kazi ili kulinda masilahi ya wafanyakazi. Alisema ni jambo lisilokubalika kuona baadhi ya wawekezaji wanawadhulumu wafanyakazi ambao wengi ni wazawa.

Hivyo ameitaka menejimenti ya kampuni hiyo ya kizalendo ishugulikie madai ya wafanyakazi na vibarua wake sanjari na kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.”Sipo tayari kuona jasho la wanyonge hawa linapotea bure,shugulikieni madai yao na ndani ya siku 21 toka leo nipate taarifa kama madai na changamoto walizoeleza zimeshugulikiwa”.

Ngubiagai aliongeza kusema tabia ya baadhi ya wawekezaji dhidi ya wafanyakazi na vibarua, hasa wazawa inasasababisha malalamiko na migogoro ya mara kwa mara. Hali ambayo licha ya kuwakafisha tamaa wananchi juu ya faida ya uwekezaji lakini pia inasababisha wachukiwe. Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Zuberi Mwalimu licha ya kuhaidi kutekeleza agizo la mkuu huyo wa wilaya ikiwamo kulipa mishahara na kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwenye mfuko wa jamii wa taifa wa jamii (NSSF) inayokadiriwa
kufikia shilingi 67.00 milioni zikiongezwa na mishahara ya wafanyakazi na vibarua.

Awali wafanyakazi na vibarua hao walimueleza mkuu huyo wawilaya hawajalipwa mishahara kwa takribani miezi saba, michango yao kutowasilishwa kwa wakati NSSF, kutolipwa malipo ya muda ya ziada, kutopewa lkiizo, kutokuwepo huduma ya kwanza katika machimbo hayo, kutofuatwa kwa taratibu na sheria za kuwaachisha kazi na kufanya kazi wiki mzima bila ya kuwa na siku ya mapumziko.

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Leave a Reply