AFYA

NAOMBA RADHI KWA VIONGOZI WOTE NILIOWATAJA KWENYE MAZUNGUMZO YANGU NA MAMA SEPETU-STEVE NYERERE.

on

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Msanii wa Filamu na Muigizaji mahiri hapa nchini Steve Nyerere, akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar kuhusiana na mambo mbalimbali yaliyotokea hivi karikuni ,likiwemo suala la ujumbe wa sauti ambao umekuwa ukisambazwa katika mitandano ya kijamii ukimuhusisha yeye Steve pamoja na Mama Wema Sepetu.

“Kulikuwa na maongezi ya simu kati ya mimi na mama Sepetu, mimi ndio nilikuwa naogea na mama Sepetu, Maneno yasipindishwe”, amesema Steve Nyerere na kuongeza kuwa yeye ana miaka 25 kwenye sanaa, inakuaje leo mtu anatoa ama anasambaza mambo binafsi waliokuwa wakiyazungumza kwa ajili ya kumsaidia Mtoto wake.

Msanii wa Filamu nchini Steve Nyerere, jana alikutana na Waandishi wa Habari, ambapo katika mkutano huo amekanusha kuwa Wasanii nchini hawakidai Chama Cha Mapinduzi fedha kwa ajili ya Mradi wa Mama Ongea na Mwanao, wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Katika Mkutano huo STEVE NYERERE amesisitiza kuwa kilichosemwa na WEMA SEPETU kuwa anaidai CCM fedha ni uongo, kwani walilipwa huku akisema Msanii aliyelipwa fedha nyingi katika kazi hiyo ni Wema Sepetu, hivyo anashangaa kusikia akidai kuwa hajalipwa.

Mradi wa Mama Ongea na Mwanao uliratibiwa na Steven Nyerere huku akisaidiwa na Wema Sepetu na kazi yake ilikuwa ni kutoa elimu kwa wazazi kuwa karibu zaidi na vijana wao wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Hata Hivyo, Steve Nyerere, ametumia mkutano huo kukiri kuwa Sauti iliyotumwa kwenye Mitandao ya Kijamii inayohusisha mazungumzo yake na Mama yake Wema Sepetu ni ya kwake, hivyo amewaomba radhi viongozi wote aliowataja katika mazungumzo hayo.

“Kulikuwa na maongezi ya simu kati ya mimi na mama Sepetu, mimi ndio nilikuwa naogea na mama Sepetu yasipindishwe,” Ile Sauti imekuja kuachiwa juzi wakati watu wanahama chama, kwanini nirekodiwe? naamini wamefanya hivyo makusudi”, alisema Steve Nyerere

“Namuomba radhi Rais Magufuli na Chama changu cha CCM, yanaongelewa mengi ninayasikia, naomba radhi familia pia, niliteleza, Nimetaja viongozi katika ile sauti halafu mtu anakuja kuisambaza nimetaja viongozi wa Nchi, Mama alichofanya amenikosea sana, Lakini namuachia Mungu” alimaliza kusema.

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply