AFYA

MANCHESTER UNITED MABINGWA WA EFL CUP 2017 (+Video)

on

Usiku wa February 26 2017 ndio majibu yalipatikana nani anastahili kuwa Bingwa wa EFL Cup 2017 kati ya Man United dhidi ya Southampton, kwa mujibu wa mitandao mingi ya England hiyo ilikuwa ni game inayozikutanisha timu bora Southampton na Man United ambao wanawachezaji bora.

Man United imefanikiwa kupata ushindi wa goli 3-2 katika game hiyo ya fainali, Zlatan Ibrahimovic anaibuka kuwa shujaa wa Man United baada ya kufunga goli dakika ya 19 na dakika ya 87 kufunga goli lililoipa ushindi Man United, huku Jesse Lingard akiifungia Man United goli la pili dakika ya 39.

Licha ya Southampton kuonesha jitihada za kusaka ushindi na kufanikiwa kusawazisha goli mbili za mwanzo kupitia kwa Manolo Gabbiadini dakika ya 45 na 49 na kuutawala mchezo kwa asilimia 52 na Man United asilimia 48, haikusaidia Southampton kupata ushindi.

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply