AFYA

NDEMANGA KULA SAHANI MOJA NA WAUZAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA LINDI

on

Na. ABDULAZIZ, LINDI

Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga ametoa onyo kali kwa wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya na matumizi ya pombe za vifungashio vya plasitiki (Maarufu viroba) na kuwataka wanafunzi kuwafichua wenzao wanaotumia vilevi wakiwa shuleni ili kupunguza athari za mtindio wa ubongo.

Ikiwa ni kumbukizi ya mwasisi na mwanzilishi wa scout Duniani, Sir Lord Baden powell  yaliyoazimishwa jana na kushirikisha wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi na sekondari, Ndemanga amekemea matumizi ya madawa hayo ya kulevya kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Akifunga maadhimisho hayo, Shaibu Ndemanga ametoa agizo kwa jamii ikiwemo wanafunzi kuepuka matumizi madawa na vileo ambapo tayari mikakati imeandaliwa kuhakikisha vijana wanakuwa kwa maadili na kuzingatia masomo yao.

Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari ya Nyangao, John Tusimwige pamoja na kukemea matumizi ya dawa za kulevya pia ameeleza kuwa shule ya sekondari Nyangao imejipanga kutoa mafunzo kwa shule mbalimbali ikiwemo walimu kuanzisha vituo vya scout ili kujenga utayari na ukakamavu kwa wanafunzi ili waweze kujitegemea.

Katika maadhimisho hayo ya siku ya scout yaliyofanyika katika uwanja wa ilulu mjini lindi yaliyoanza kwa maandamano na burudani mbalimbali Baadhi ya wanafunzi wa Nyangao sekondari waliuunga mkono jitihada za waziri mkuu Kassim Majaliwa kuzuia utengezaji wa pombe za viroba pamoja na Serikali kupambana na madawa ya kulevya nchini.

Nae Mkurugenzi wa manispaa ya lindi, Jomaary Mrisho Satura akimkaribisha mkuu wa wilaya kufunga maadhimisho hayo aliahidi kutoa ushirikiano kwa kusaidia uanzishaji wa scout katika shule zilizo katika Manispaa ya lindi.

Katika kuwasilisha ujumbe mabango mbalimbali ya wanafunzi ya wanafunzi waliopita mbele ya mgeni rasmi walitoa msisitizo dhidi ya hatua ya serikali kupiga vita madawa ya kulevya na matumizi ya viroba ikiwemo ujumbe kwa njia ya sanaa.

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply