AFYA

RICH MAVOKO AKABIDHIWA CERTIFICATE AWARD YA JIWE LA MWEZI.

on

Msanii Rich Mavoko kutoka kwenye lebel ya Wasafi Classic Baby (WCB)  amesema ni heshima kubwa sana kwa wimbo wa KOKORO kupewa certificate Kama jiwe bora la mwezi.

Certificate hiyo ya Recognition Awards alikabidhiwa jana mjini Moshi mbele ya mashabiki wa kipindi cha Xxl waliojitokeza kushuhudia matangazo Mubashara yaliofanyika siku ya jana.

Certificate hiyo ambayo hutolewa na Kipindi namba moja cha Burudani East and Central Africa cha Xxl ndani ya Superbrand radio station Clouds Fm.

Certificate ya jiwe la Mwezi ni mahususi kwa kutambua ubora wa kazi za wasanii na juhudi zao katika shughuli zao za kisanaa.

“Tunawataka wasanii wafanye kazi nzuri kitu kizuri siku zote kinaonekana kwenye macho ya kawaida na hufika mbali zaidi na wasanii wasibweteke”, alizungumza Brand Manager wa Xxl, Born To shine mtangazaji BDozen.

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply