AFYA

SHAMSA FORD ATOA USHAURI HUU KWA WASANII WA KIKE BONGO

on

Msanii wa Filamu nchini Mwanadada Shamsa Ford ametoa ushauri kuntu kwa wasanii wenzake wa kike hususani waigizaji wa Filamu wa kuwataka waolewe.Shamsa Ford akizungumza kwenye kipindi cha Double XL cha Clouds FM amesema wanawake wengi walio kwenye Tasnia hiyo wanasubiri mpaka wapate mabwana wenye pesa ndiyo wakubali kuolewa,kumbe hawajui hata hizo mali walizonazo hawajazipata peke yao hivyo amewashauri kukubali kuolewa na mwanaume yeyote ambae atampenda kwa hali yoyote aliyonayo.

“Mimi nawashauri wasanii wenzangu wa kike wakimpata mtu mwenye mapenzi ya dhati ni bora kuolewa tuu,kwani kusubiri mpaka kumpata mwanaume tajiri aje akuambie anakupenda !! ndio ukubali bila kujua tayari kuna mtu katoka nae mbali mpaka kuwa tajiri kwahiyo nawashauri msichague chague wanaume itawa cost” amesema Shamsa Ford.

__________________________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you