AFYA

HALMASHAURI YA WILAYA YAJIZATITI KUENDELEZA MAPAMBANO DHIDI YA VVU

on

Na. Ahmad Mmow, Lindi.

BAADA ya kufanikiwa kupunguza maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa 5%. Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi imeahidi kulinda na kuendeleza mafanikio hayo. Ahadi hiyo imetolewa mwanzoni mwa wiki hii na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Ahmad Makoroganya alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari mjini Nachingwea  waliotaka kujua mchango na mipango ya halmashauri hiyo kuhusu mapambano dhidi ya UKIMWI.

Makoroganya alisema baada ya wilaya hiyo kufanikiwa kupunguza maambukizo kutoka 6.8% ya mwaka 2008 hadi 1.8% ya 2016. Halmashauri hiyo italinda na kuendeleza mfanikio hayo kwa kutumia rasilimali ilizonazo ikiwamo fedha zinazotokana na vyanzo vya mapato yake ya ndani.

Makoroganya alisema kwakutambua miongonoi mwa sababu zinazochangia kuwepo maambukizi ya VVU ni umasikini walionao baadhi ya vijana na wanawake, halmashauri hiyo imekuwa ikipeleka fedha kwa wakati kwa vikundi vya ujasiriamali vya makundi hayo.

“Tunatambua na kuthamini kazi kubwa iliyofanywa na tume ya  taifa ya kudhibiti UKIMWI, kupitia mfuko wa taifa wa kupambana na UKIMWI. Hata hivyo sisi kwa upande wetu tunawajibu wa kuchangia mapambano hayo na tuendeleza mafanikio yaliyopatikana baada ya ufadhili wa tume hiyo kumaliza muda wake,” alisema Makoroganya.

Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba hadi sasa halmashauri hiyo imefikisha kwa makundi hayo takribani shilingi 260.00 milioni zilizotokana na mapato yake ndani. Ikiwa ni katika kipindi cha robo tatu ya mwaka wa fedha wa 2016/2017. Ambapo katika mwaka huu wa fedha ilitenga takribani shilingi 9.00 milioni kwa ajili ya matumizi ya vita ya mapambano dhidi ya UKIMWI.

“Fedha zilipelekwa kwa vikundi vya wanawake na vijana ni 10% ya makusanyo ya ndani yaliyokusanywa katika kipindi cha robo tatu ya mwaka wa fedha tulionao. Ni asilimia miamoja ya fedha zilizotakiwa kupelekwa kutokana kwa mujibu wa fedha zikizokusanywa,” aliongeza kusema Makoronya.

Akieleza baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kuanzia mwaka 2008 ambao halmashauri hiyo ilianza kupokea fedha kutoka mfuko wa taifa wa mapambano dhidi ya UKIMWI, mratibu wa mapambano dhidi ya UKIMWI wa halmashauri hiyo, Fatuma Milao, alisema fedha hizo zimewezesha uhamasishaji na utoaji elimu na stadi za maisha kwa vijana na makundi mengine ya kijamii. Ikiwamo mahali pa kazi. Hususani kwa watumishi wa halmashauri hiyo.

Alisema katika halmashauri hiyo kuna vikundi 27 vya watu wanaoishi na VVU. Ambapo vikundi 22 kati ya hivyo vimepatiwa mafunzo ya ujasiriamali. Alisema licha ya vikundi hivyo lakini pia limeundwa baraza la watu wanaoishi na VVU ambalo linafanya shuguli zake kwa ukaribu na halmashauri ya wilaya. Ikiwamo utoaji elimu na uhamasishaji kuhusu mapambano hayo amayo yanaelekea kufanikiwa katika wilaya hiyo.

Nae mwenyekiti wa baraza la watu wanaoishi na VVU, Zubeda Ungele alisema  elimu inayotolewa imesababisha  kupitia matamasha na mikutano imesababisha maambukizi kupungua. Hata hivyo Zubeda alisema bado elimu inahitajika. Hasa kuhusu unyanyapaa.

“Bado kuna tatizo la unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na VVU, lakini pia dawa zinazozuia magonjwa nyemelezi ziwe zinapatika kwa wakati maana nalo ni changamoto. Muda mwingine tunalazimika kununua,” alisema Ungele.

Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa hosipitali ya wilaya ya Nachingwea, Dkt Ibrahim Pazia, alisema hali ya maambukizi imepungua kwa kiasi kikubwa wilayani humo. Kwani mwaka 2008 kiwango cha maambukizi kilikuwa 6.8, hata hivyo hadi kufikia mwaka 2016 kiwango hicho kimeshuka nakufikia 1.8%.

Alitaja sababu za kushuka kwa kiwango cha maambukizi kuwa ni jamii imebadili mtazamo. Hivyo watu wengi wamebadili tabia na kuanza kupimwa afya zao.

“Watu wengi hawakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu UKIMWI. Matumizi ya mipira ya kinga (kondomu) ni makubwa, siku za nyuma  boksi tatu tu zilikuwa zinatumika kwa muda mrefu. Lakini sasa zinatumika hadi boksi 7, hiyo inaonesha ni kwakiasi gani watu walivyobadilika na kuchukua tajadhari,” alisema Dkt Pazia.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Rukia Mwango, alisema anatambua kuwa ugonjwa huo unapunguza nguvu kazi ya taifa kwasababu waathirika wakubwa ni vijana. Hivyo atahakikisha 10% ya fedha za halmashauri zinazotokana na vyanzo vyake vya ndani zinapelekwa kwa wakati katika vikundi vya wanawake na vijana. Huku akihaidi katika mikutano na vikao vyake, agenda ya vita dhidi ya UKIMWI haitakosekana.

_________________________________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you