AFYA

RAIS MAGUFULI AANZA ZIARA KATIKA MIKOA YA PWANI, LINDI NA MTWARA

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe. Dkt.  John Pombe Magufuli, Jana tarehe 02 Machi, 2017 ameanza ziara ya kikazi ya siku 4 katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.
Katika ziara hiyo Mhe. Rais Magufuli atafungua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.
Jana asubuhi Mhe. Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd. kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani na baadaye akaelekea Mkoani Lindi.
Tarehe 03 Machi, 2017 Mhe. Rais Magufuli ataendelea na ziara yake Mkoani Lindi na kesho kutwa tarehe 04 Machi, 2017 atafanya ziara yake Mkoani Mtwara.
_________________________________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana