AFYA

VIDEO: MANCHESTER UNITED WASALIA NAFASI YA 6, BAADA YA SARE DHIDI YA BOURNEMOUTH

on

Manchester United Leo wameshindwa kung’oka Nafasi ya 6 baada kutoka 1-1 na Mtu 10 Bournemouth kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.

Man United walifunga Bao lao Dakika ya 23 baada ya Kona kushindwa kuokolewa vizuri na Valencia kuachia Shuti ambalo Marcos Rojo akaliparaza na Mpira kutinga.

Bournemouth walisawazisha Dakika ya 40 kwa Penati ya Joshua King ambae aliwahi kuchezea Timu za Vijana za Man United. Penati hiyo ilitolewa na Mwamuzi Kevin Friend kwa madai Phil Jones kamwangusha Pugh.

Dakika chache kabla Haftaimu kulitokea rabsha Uwanjani wakati Mings alipomtimba Kichwani Ibrahimovic na muda mdogo baadae Kona ya Man United alirukiwa na Ibrahimovic na kiwiko chake kumpiga Kichwani Mings.

Matukio hayo yalileta mjadala Mrefu lakini Wachezaji hao Wawili wakaepuka Kadi na Surman wa Bournemouth kupewa Kadi Njano bila ya Refa kutambua Mchezaji huyo alikuwa tayari anayo Kadi ya Njano na Dakika kadhaa baadae Refa Friend akakumbuka kumpa Surman Kadi Nyekundu na hivyo Bournemouth kubaki Mtu 10.

Hadi Haftaimu Man United 1 Bournemouth 1.Dakika ya 69 Jose Mourinho alibadili Wachezaji Watu Watatu kwa mpigo kwa kuwaingiza Marouane Fellaini, Jesse Lingard na Marcus Rashford badala ya Wayne Rooney, Luke Shaw na Michael Carrick.

Dakika 2 baadae Man United walipata Penati baada ya Krosi ya Pogba kushikwa na Smith lakini Penati hiyo iliyopigwa na Ibrahimovic kuokolewa na Kipa Boruc.

Hadi mwisho Man United 1 Bournemouth na Man United kubaki hapo hapo Nafasi ya 6 wakifungana Pointi na Liverpool ambao wako Nafasi ya 5.

VIKOSI: Manchester United (Mfumo 4-2-3-1): De Gea; Valencia, Jones, Rojo, Shaw; Carrick, Pogba; Mata, Rooney, Martial; Ibrahimovic.

Akiba: Romero, Blind, Smalling, Fellaini, Herrera, Lingard, Rashford.

AFC BOURNEMOUTH (Mfumo 4-4-2): Boruc; A Smith, S Cook, Mings, Daniels; Fraser, Arter, Surman, Pugh; Afobe, King.

Akiba: Allsop, Cargill, B Smith, Gosling, Ibe, Wilshere, Gradel.

REFA: Kevin Friend

_______________________________________________________

PAKUA APPLICATION YETU KUPATA HABARI ZETU KWA HARAKA KWA KWENDA PLAYSTORE NA SEARCH LINDI YETU, AU BOFYA LINK HII HAPA

DOWNLOAD LINDI YETU APPLICATION

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you