AFYA

ARSENAL NJE UEFA CHAMPIONZ LIGI BAADA YA KUPIGWA 10 – 2

on

ARSENAL wakiwa kwao Emirates Jijini London kucheza Mechi ya Pili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, huku wakihitajika kupindua kipigo cha 5-1 cha Mechi ya Kwanza ili kutinga Robo Fainali, walijikuta wakitwangwa tena Bao 5-1 na Bayern Munich.Hivyo Bayern Munich wanasonga Robo Fainali kwa Jumla ya Bao 10-2 kwa Mechi mbili. Huu ni Msimu wa 7 mfululizo kwa Arsenal kushindwa kuvuka Hatua hii ya UCL.

Arsenal walianza Mechi hii kimkosi pale Mchezaji wao Danny Welbeck, aliepangwa kuanza Mechi, kujiondoa baada ya kujisikia Mgonjwa wakati wa kupasha moto kabla Mechi kuanza na nafasi yake kuchukuliwa na Olivier Giroud. Lakini Dakika ya 19, Theo Walcott akawapa Arsenal Bao la kwanza kwa Shuti kali lililomshinda Kipa Neuer.Hadi Haftaimu, Arsenal 1 Bayern 0.

Dakika ya 52 Sentahafu wa Arsenal Koscielny alimwangusha Lewandowski na Refa kutoa Penati na pia kumpa Kadi Nyekundu. Penati hiyo ilifungwa na Lewandowski na Gemu kuwa 1-1.

Kuanzia hapo Mvua ya Magoli ya Bayern ikashuka kwa kupiga Bao nyingine 4 Dakika za 68, 78, 80 na 85 kupitia Arjen Robben, Douglas Costa na Arturo Vidal, Bao 2.Hadi Mpira kumalizika, Arsenal 1 Bayern 5.

VIKOSI: Arsenal: Ospina, Bellerin, Mustafi, Koscielny, Monreal, Ramsey, Xhaka, Walcott, Oxlade-Chamberlain, Giroud, Sanchez.
Akiba: Cech, Gibbs, Gabriel, Coquelin, Ozil, Lucas

Bayern Munich: Neuer, Rafinha, Martinez, Hummels, Alaba, Alonso, Vidal, Thiago, Robben, Lewandowski, Ribery.
Akiba: Ulreich, Costa, Bernat, Muller, Coman, Kimmich, Sanches.

______________________________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you