AFYA

BREAKING NEWS: DJ FETTY KUREJEA CLOUDS FM KESHO NDANI YA XXL

on

Dunia inaadhimisha mchango na thamani ya Wanawake duniani kila inapofika Tarehe 8 March kila mwaka. Kila nchi  inakuwa na utaratibu wake wa namna gani wa kusherehekea ama kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani Wapo Wanawake wengi ambao wameleta alama chanya ya mabadiliko kwenye tasnia mbalimbali ikiwepo tasnia ya Burudani. Huwezi kuwataja kwa majina Wanawake wote ila wapo wengi ambao walileta mabadiliko yakaonekana kwa kile  walichokuwa wanafanya.

Clouds Fm kulikuwa na sauti moja nzuri hivi katika Dakika 180 katikati ya wanaume wawili wakorofi in town, Ushajua namzungumzia nani eeeh! Basi vunga Kama umeshamfahamu niwatonye washkaji ambao hawakubahatika kumsikiliza sauti yake.

Binti wa kisukuma Fatma Hassan muite Dj Fetty ukipenda Kwefeee siku ya kesho atakuwepo mjengoni kuiongoza show namba moja ya kijanja XXL kuadhimisha siku ya Wanawake duniani.

Dj Fetty ambaye aliondoka Clouds  mwaka 2015 baada ya kuomba kupumzika aendelee na mishemishe zake siku ya kesho atakuwepo mjengoni kupiga show along side Mammi Babbie pamoja na Dj Sinyorita! Kukamilisha mzunguko kamili wa #MalkiaWaNguvu

Dj Fetty ni baadhi ya Madj wakike wachache walioweka hamasa kwenye game ya bongo Fleva na kutoa nafasi ya kuzaliwa Madj wengine wakike kufuata nyanyo kwenye  Udj!

Kesho inapofika Saba kamili mchana Tune your Favourite Station Clouds Fm kuisikia sauti ya Dj Fetty.

Dj fetty kesho anarejea mjengoni kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani na kuonyesha kizazi kipya ubunifu wa Enzi zake je sauti ile ipo ama ishapotea.

____________________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you