AFYA

LIWALE YATENGA SHILINGI 20.00 MILIONI KUPAMBANA NA UKIMWI.

on

Na.Ahmad Mmow, Liwale.

KATIKA kuhakikisha inalinda na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana kwa kutumia fedha za mfuko wa tume ya taifa ya kupambana UKlMWI. Halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi, imepitisha na kutenga shilingi 20.00 milioni kutoka kwenye bajeti yake ya mwaka wa fedha wa 2017/2018. Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa halmshauri hiyo, Justine Monko, alipokuwa anazungumzia mafanikio na changamoto zilizopo katika mapambano dhidi ya UKIMWI. Mwishoni mwa wiki iliyopita, mjini Liwale.

Monko alibainisha kwamba halmashauri hiyo inatambua kwamba baada ya tume ya taifa ya kudhibiti UKIMWI kumaliza muda wake wa kufadhili fedha kwa ajili mapambano hayo, jukumu la kuendeleza mafanikio yaliyotokana na ufadhili huo lipo mikononi mwa halmshauri yao. Hivyo imeptisha na kutenga kiasi hicho cha fedha kitakachotokana na vyanzo vya mapato vya ndani ya halmashauri hiyo. Alisema sanjari na kutenga kiasi hicho maalum kwa mapambano hayo, lakini pia itaendelea kupeleka 10% ya mapato yake ya ndani katika vikundi vya ujasiriamali vya vijana na wanawake ilikuwajengea uwezo wa kiuchumi.

Monko alisema juhudi kubwa zilizofanyika kwa kutumia fedha za tume ya taifa ya kudhibiti UKIMWI zimesababisha kupungua maambukizi ya Virusi vya UKIMWI katika wilaya hiyo.

“Lakini katika kufanikisha azima yetu tutalitazama zaidi suala la kufikisha elimu kwa jamii. Tumeanza kuvisaidia vikundi maalam vya mapambano dhidi ya UKIMWI ambavyo vimekuwa na mchango mkubwa katika kufikisha elimu kupitia sanaa za maonesho kwenye matamasha na mikutano. Tutalisaidia pia baraza la watu wanaoishi na VVU, sanjari na vikundi vya wa VIU ambavyo navyo vinamchango mkubwa katika kutoa elimu,” alisema Monko.

Mratibu wa mapambano dhidi ya UKIMWI wa halmashauri hiyo, Moses Mkoveke, alisema maambukizi ya VVU katika wilaya hiyo kuanzia mwaka 2008 hadi 2016 yamepungua kwa 4%. Kwani mwaka 2008 kiwango cha maambukizi kilikuwa 6%. Hata hivyo hadi mwezi Desemba mwaka jana kiwango hicho kilishuka nakufikia 2%.

Mkoveke alizitaja baadhi ya shuguli na juhudi zilizofanyika kwa kutumia fedha za tume ya taifa ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) ni kufanikiwa kutengeneza kamati za kinga dhidi ya UKIMWI katika vijiji na kata zote za wilaya hiyo, kuunda vilabu vya mapambano dhidi ya UKIMWI, kuvijengea uwezo vikundi vya sanaa ambavyo vinatoa elimu kwenye matamasha. Ambapo hadi sasa kunavikundi 20. Aliongeza kusema wataendelea kutoa semina kwa vikundi vya mapambano dhidi ya UKIMWI (vilabu) na kuvipatia mitaji.

“Hilo tumelinza tayari, klabu ya sekondari ya Nicodemus Banduka imewezeshwa na imeanzisha mradi wa kufuga kuku. Pia kinamradi wa kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ili kuihamasisha jamii ione umuhimu wa kupanda miti,” alisema Mkoveke.

Mratibu huyo aliyashukuru mashirika yasio ya kiserikali ikiwamo Save the chidren.

“Fedha za TACAIDS zilisaidia sana katika bajeti ya shuguli za utoaji elimu ya kupambana na kuzuia maambukizi mapya, lakini mashirika yasio yakiserikali yalisaidia dawa na chakula na mengine kusambaza chakula bora kwa wa VIU”, aliongeza kusema Mkoveke.

Kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Liwale, Dkt Maulid Majala, alisema wanajukumu kubwa la kuendelea kutoa elimu ili jamii iendelee kubadili mitazamo na kujikinga dhidi ya maambukizi, kupima afya kwa hiari na kwa wanaoishi na VVU kuhudhuria kwenye vituo vya kutolea huduma kwa wakati. Ambapo wanajipanga ilikuhakikisha kiwango cha maambukizi kinapungua na kufikia 0%.

____________________________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you