AFYA

UEFA CHAMPIONZ LIGI :: MABINGWA REAL MADRID WAIBONDA NAPOLI 6-2

on

LEO Mabingwa Watetezi Real Madrid, wakiwa Ugenini huko Stadio San Paolo Mjini Napoli Nchini Italy, walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa Napoli 3-1 katika Mechi ya Pili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, na hivyo kutinga Robo Fainali kwa Jumla ya Bao 6-2 kwa Mechi 2.Dakika ya 24 Napoli walienda 1-0 mbele kwa Bao la Dries Mertens. Bao hilo lilidumu hadi Mapumziko.

Dakika ya 52 Kona ya Toni Kroos ilifungwa kwa Kichwa na Sergio Ramos na Gemu kuwa 1-1. Dakika ya 57 Kona nyingine ya Kroos ilimaliziwa na Ramos na Real kuandika Bao la Pili.Real walipiga Bao lao la 3 Dakika ya 90 baada ya Shuti la Cristiano Ronaldo kuokolewa na Kipa Reina na Alvaro Morata, alietokea Benchi, kuukwamisha Mpira huo uliotemwa.Hadi mwisho Napoli 1 Real 3.

VIKOSI: NAPOLI: Pepe Reina, Alexander Soderlund, Raul Albiol, Kalidou Koulibaly, Faouzi Ghoulam, Allan, Amadou Diawara, Marek Hamsik, Jose Callejon, Dries Mertens, Lorenzo Insigne

Akiba: Rafael Cabral Barbosa, Jorginho, Christian Maggio, Nikola Maksimovic, Piotr Zielinski, Marko Rog, Arkadiusz Milik

REAL MADRID: Keylor Navas, Dani Carvajal, Pepe, Sergio Ramos, Marcelo, Toni Kroos, Casemiro, Luka Modric, Gareth Bale, Karim Benzema, Cristiano Ronaldo

Akiba: Nacho, James Rodriguez, Kiko Casilla, Lucas, Alvaro Morata, Isco, Danilo

REFA: Cuneyt Cakir [Turkey]

__________________________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you