AFYA

METHOD MWANJALI WA SIMBA KUWA NJE YA UWANJA MWEZI MZIMA

on

Mchezaji wa klabu ya Simba, Mzimbabwe Method Mwanjali ataendelea kuwa nje kwa mwezi wote wa Machi kutokana na maumivu ya goti.

Mwanjali hajajumuishwa katika kikosi ambacho kimeenda ziarani mkoani Dodoma kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji, Polisi Jumamosi wiki hii Uwanja wa Jamhuri.

Daktari wa klabu ya Simba, Yassin Gembe amesema kwamba Mwanjali hatakwenda Dodoma na hatahusishwa kwenye programu yoyote ya timu mwezi huu wa Machi.

Gembe amesema kwamba wanataka Mwanjali aendelee kupatiwa matibabu hadi awe fiti kabisa, ili akirejea iwe amerudi rasmi kuisaidia timu.

“Tunataka apone vizuri kabisa ndiyo arejee uwanjani. Kwa hiyo Machi yote hatakuwemo kwenye programu za timu,” amesema Gembe.
Mwanjali aliumia goti katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Prisons Februari 11, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ikishinda 3-0.

Mwanjali aliye katika msimu wake wa kwanza Simba SC, alitolewa kwa machela siku hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Mwinyi Kazimoto dakika ya 62.

Source: Binzubeiry

___________________________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you