AFYA

MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA LINDI SELEMANI METHEW APATA DHAMANA, ATAKA WANASIASA KUACHA SIASA ZA CHUKI

on

Na. Ahmad Mmow, Lindi.

Mwenyekiti wa mkoa wa Lindi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Seleman Methew, amesema kazi ya siasa hivi sasa ni ngumu kuliko miaka ya nyuma. Methew aliyasema hayo, leo mjini Lindi alipoongea na Lindiyetu.co.tz jinsi alivyopokea uamuzi wa mahakama ya rufaa wa kumpa dhamana baada ya kuhukumiwa na mahakama ya hakimu mkazi ya mkoa wa Lindi kifungo cha miezi nane.

Methew alisema siasa zimekuwa ngumu kuliko miaka ya nyuma kutokana na baadhi ya viongozi kuwafuatafuata kwa lengo la kuwakomoa watu ambao wanawaona ni tishio kwa nafasi zao pindi wanapowaona wanawahudumia wananchi. Alisema hakuna mwanasiasa mwenyenia njema ya kuwahudumia wanananchi anaependa kuvunja sheria za nchi. Bali kinachofanyika ni fitina chafu za kisiasa ili waonekane wakorofi na wasiopenda amani. Japokuwa mambo wanayofanya yanamasilahi kwa wananchi.

Mwenyekiti huyo alisema yeye alikuwa anatekeleza kwa vitendo agizo la Rais Magufuli, aliyesema uchaguzi umekwisha, kilichobaki ni kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

“Mimi siku mbili kabla sijakamatwa nilikuwa naendelea kuchimbisha visima vya maji katika baadhi ya vijiji vyenye shida ya maji katika jimbo la Mtama, ambalo katika uchaguzi uliopita niligombea ubunge, nilikuwa natekeleza kwa vitendo agizo na kauli mbiu ya Rais ya kufanya kazi,” alisema Methew.

Mwenyekiti huyo ambae amewahi kuwa diwani wa kata ya Vijibweni wilaya ya Kigamboni, kupitia CCM. Katika mazungumzo hayo hakusita kuwamwagia sifa Rais Magufuli, makamo wa Rais na waziri mkuu kwa jinsi wanavyofanya kazi ya kuwatumikia wananchi bila kuchoka. Alisema viongozi hao wanafanya kazi vizuri sana na wanania thabiti ya kuwatumikia wananchi na kuipeleka nchi mbele kimaendeleo.

Hata hivyo wanaangushwa na baadhi ya watendaji wa ngazi za chini, ambao wanashindwa kuwasadia. Badala yake wanawaacha peke yao wakihangaika huku na kule.

“Hawawasaidii kabisa, kwasababu wamekosa ubunifu. Badala yake wamekuwa watu wakusubiri maagizo tu,” alisema.

Akizungumzia mustakabari wake kisiasa baada ya kukutana na kadhia hiyo iliyomfanya akaejela kwa takribani miezi mitatu baada ya kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha miezi nane. Alisema kilichomtokea ni gharama ya kazi ya siasa ambayo yeye kwa hiari yake ameamua kuifanya kwa moyo mmoja. Kwahiyo hatarurdi nyuma bali ataendelea kuifanya kwa kuzingatia taratibu na sheria za nchi.

“Nilikuwa mchezaji wa mchezo wa soka, nilitoa mchango wangu wa ujenzi wa taifa kupitia kazi hiyo. Nilipostahafu nikaamua nifanye kazi ya siasa, wenzangu wamekuwa walimu wa mchezo huo na wengine wanafanya kazi nyingine walizoamua kufanya,” alibainisha Methew.

Alitoa wito kwa viongozi wenyetabia ya kufanya siasa za chuki na visasi visivyo nasababu waache tabia hiyo. Bali washirikiane kuwatumikia wananchi kwa kushindana kuwahudumia. Badala ya kukomoana. Jana mahakama ya rufani ilikubali ombi la kupewa dhamana mwenyekiti huyo na katibu wa CHADEMA wa tawi la Nyangamara, Ismail Kupilila.

_______________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you