AFYA

RC SHIGELLA AITAKA TEMESA KUMPATIA ORODHA YA WADAI SUGU

on

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella akisisitiza jambo wakati akifungua kikao cha Bodi ya Barabara (Road Boad) ambapo alisisitiza umuhimu wa wabunge wa mkoa wa Tanga kutumia nafasi zao kusaidia kuelezea changamoto zinazozikabili barabara zetu ili zipewe msukumo.Meneja wakala wa barabara Mkoani Tanga (Tanroad) Mhandisi Alfred Ndumbaro akisisitiza jambo kwenye kikao hicho kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu.Meneja wa Temesa Mkoa Mhandis Margareth Gina akitolea ufafunzi baada ya maswali yaliyoulizwa na wajumbe wa kikao hicho Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akifuatilia kwa umakini kikao hicho.Wajumbe wakifuatilia hoja zilizoainishwa kwenye makabrasa kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kilindi (CCM) Omari Kigua na Mkuu wa wilaya ya Kilindi Sauda Mtondoo

Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

WAKALA wa Ufundi na Umeme Mkoani Tanga (Temesa) wameagizwa kuwasilisha orodha ya majina ya wadaiwa sugu wa taasisi mbalimbali za serikali kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa ikiwemo kuharakisha ulipwaji wake.

Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela wakati wa kikao cha kwanza cha Bodi ya barabara mkoani hapa ambapo alisema wao kama serikali ya mkoa hawapo tayari kuona wakala huyo akishindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo kutokana na juhudi zao kurudishwa nyuma kimaendeleo.

Katika kuhakikisha suala hilo linapata mafanikio makubwa yenye tija alimtaka Meneja wa wakala wa Ufundi na Umeme (TEMEMSA) Mkoa Tanga, Mhandisi Margareth Gina kumpelekea idadi ya wadaiwa sugu na taasisi hiyo ili kuweza kuangalia namna ya kuweza kupata malipo yao.

Hatua hiyo inafuatia taarifa ya Meneja wa Temesa Mkoa kuonyesha zipo taasisi nyingi za Serikali zinazodaiwa fedha nyingi bila kuwepo jitihada zozote za ulipwaji wa madeni hayo huku tasisi hizo zikiendelea kupatiwa huduma na taasisi hiyo ya Serikali.

Alisema ifike wakati kwa taasisi zote za umma zinazopata huduma kutoka kwa wakala huyo wa ufundi na umeme wahakikishe wanalipa madeni yao kwa wakati kabla majina hayo ya wadaiwa hao sugu hayajawekwa hadharani.

Mkuu huyo alisisitiza umuhimu wa majina ya wadaiwa wote sugu yaorodhoshwe bila ya kuoneana aibu na taasisi za Serikali ambazo zinadaiwa kuwa ndio vinara wakubwa wa kudaiwa ili kuweza kuangalia namna ya kupunguza madeni hayo ambayo ni hatari kwa ukuaji wa wakala huyo.

Awali akizungumza katika kikao hicho, Meneja wa Temesa Mkoa Mhandisi Margareth Gina alisema temesa imekuwa ikitoa huduma bora kwa taasisi za Serikali kutokana na kuwepo na wataalamu wengi waliobobea katika fani mbalimbali huku wakishindwa kufikia malengo kutokana na kutolipwa
na wateja wao.

Mhandisi Gina alisema ipo orodha kubwa ya majina ya wadaiwa sugu ambapo ipo haja ya kuyaweka hadharani kama Mkuu wa Mkoa alivyoagiza na kufanya hivyo kunaweza kusaidia kwa namna moja au nyingine kuweza na kukusanya madeni hayo.
“Zipo taasisi za serikali zanadaiwa hadi milioni 100 na orodha yote ya wadaiwa sugu ninayo na naweza kuyataja ila naona itakuwa kufedheheshana tu mbele ya kikao hiki”Alisema.

Aidha alisema taasisi za Serikali kwa asilimia kubwa zimekuwa miongoni mwa wateja wanaoikwamisha temesa kuendelea na ufanisi wa shughuli zake jambo ambalo linatakiwa litafutiwe ufumbuzi na wa haraka kukomesha tabia hiyo iliyozoeleka.

Kwa upande wake, katibu Tawala Mkoa Tanga Mhandisi Zena Saidi alisema hakuna sababu ya kuficha wanaodaiwa lazima waorodheshwe na walipe madeni yao kwa wakati ili temesa iweze kuendelea na majukumu yake.

_________________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you