AFYA

SOPHIA SIMBA, MADABIDA WAVULIWA UANACHAMA CCM. EMMANUEL NCHIMBI APEWA ONYO KALI

on

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amesema kuwa kikao cha Halmashauri kuu ya Taifa CCM, kimeazimia kwa kauli moja kuwafukuza uanachama baadhi ya wanachama wake akiwamo Aliyekuwa Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa wanawake CCM Taifa Mh.Sophia Simba, Ramadhani Madabida pamoja na wenyeviti mbalimbali wa mikoa nchini.

Ndg. Emmanuel Nchimbi amepewa onyo kali na anatakiwa kuomba radhi wanachama na uongozi wa CCM. Josephine Genzabuke(Mb) amepewa onyo kali na pia anapoteza sifa ya kushiriki uchaguzi ujao ndani ya CCM.

WALIOFUKUZWA UANACHAMA WA CCM KUANZIA LEO:

VIONGOI WA JUMUIA

 1. Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Sophia Simba (MB)

WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU TAIFA

 1. Ally Khera Sumaye – MNEC – Babati
 2. Mathias Erasto Manga – MNEC – Arumeru

WALIOPEWA ONYO KALI

 1. Alli Mchumo – MNEC – Kilwa

WALIOACHISHWA UONGOZI.

 1. Ajili Kalolo – MNEC – Tunduru
 2. Hassani Mazala – MNEC – Singida Mjini
 3. Valerian Allen Buretta – MNEC – Kibaha Vijijini

WENYEVITI WA MIKOA (WALIOFUKUZWA)
1. Dar es Salaam Ndg Ramadhan Madabida
2. Iringa Ndg Jesca Msambatavangu
3. Mara na Ndg Christopher Sanya
4. Shinyanga Ng Erasto Izengo Kwilasa

WENYEVITI WA WILAYA (WALIOFUKUZWA).

 1. Omari Awadhi – Gairo
 2. Ally S. Msuya – Babati
 3. Makolo S. Laizer – Longido
 4. Abeid Kiponza – Iringa Mjini
 5. Salumu Kondo Madenge – Kinondoni
 6. Wilfred ole sollel Mollel – Arusha

WALIOPEWA ONYO KALI.

 1. Muhaji Bushako – Muleba

WALIOACHISHWA UONGOZI.

 1. Assa Simba Haroun – Ilala
 2. Hamisi J. Nguli – Singida Mjini

Makada takribani 40 wa chama cha mapinduzi wamepewa adhabu na adhabu zote zilizotolewa leo hazina rufaa, kamati kama hii iliyopitisha panga bara pia imeundwa visiwani ikiongozwa na Shamsi Vuai na mama Zakia Meghji na itakuja na majibu.

__________________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you