AFYA

ALIKIBA ATUPA JIWE GIZANI AMESEMA HATI MAZOEA, JE NIJIBU KWA DIAMOND?

on

March 14, 2017 Msanii na C.E.O wa WCB Diamond Platnumz aliweza kuuambia uma wa watanzania kupitia kipindi cha 360 kinachorushwa hewani na Clouds Tv kuwa hana tatizo lolote na Alikiba au watu wengi wanavyopenda kumwita King Kiba.

Diamond alisema kuwa matatizo yaliyokuwepo yalishaisha kwani walishakutana na kuongea na Kumaliza tofauti zao lakini Media bado zinafanya jitihada za kuonesha kuwa bado kuna tofauti kati yao, aliongeza kuwa angependelea Msanii alikiba angeweza kupeleka kazi zake za kisanii ilikuuzwa kwenye mtandao wake wa wasafi.com .

Kufuatia kaulihiyo kupitia mtandao wa Instagram Alikiba aliweza kupost Jumbe ambazo zimetafsiriwa kuwa nimajibu kwa msanii huyo. Ujumbe wa Kwanza ulikuwa ukisomeka: “Umeshatibua Mavumbiee Unatafuta Pa kuhemeaaa ? #KingKiba” . Baada ya Lisaa limoja baadae msanii huyo akautupia ujumbe mwingine huku wakati huu ujumbe huo ukisomeka “Waambie Wasituzoee kabisa MAZOEA kuzoeana ?? @billnass #alikibaworldtour2k17  #KingKiba” hapo akionekana kuimba mistari ya wimbo wa msanii Billnass ambaye alimtag katika Post Hiyo.

Nini Maoni yako Juu ya Jumbe Hizi, Tuachie Comment Hapo chini.

______________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you