AFYA

SINGIDA UNITED YAMREJESHA PLUIJM KATIKA NYUMBA ALIYOTIMULIWA

on

IKIWA ni baada ya saa kadhaa kupita tangu uongozi wa Singida United kuingia mkataba wa miaka miwili na Mholanzi Hans Pluijm, uongozi huo umemlipia kodi ya pango aliyokuwa anadaiwa hadi kufikia hatua juzi kutupiwa virago nje na mmiliki wa nyumba hiyo.

Yanga ndio iliyompangishia nyumba hiyo lakini imeelezwa kushindwa kulipa kodi kwa miezi kadhaa hadi kocha huyo alipovunjiwa mkataba hivi karibuni.

Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam zilieleza kuwa Singida United wameamua kubeba jukumu hilo kwa kumalizana na mwenye nyumba na kwamba mizigo ya Pluijm itaendelea kuwepo hapo hadi pale atakapoanza kazi rasmi mjini Singida na yeye kuhamia huko.Katibu Mkuu wa Singida United, Abdulrahiman Sima amekiri juu ya hilo akisema, “Pluijm alipata matatizo kwenye nyumba aliyopangishiwa, tulienda na kukutana na mhusika wa nyuma na kumalizana, hivyo atakuwepo hapo hadi baadaye atakapokuja rasmi kuanza kazi,”.

Pluijm ataondoka siku yoyote kwa ajili ya mapumziko kabla hajarejea rasmi kuanza kazi ya kuinoa timu hiyo inayoonyesha kujipanga vilivyo kuelekea michuano ya ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17.

______________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana