AFYA

HALMASHAURI KUWABURUZA MAHAKAMANI VIKUNDI VISIVYOREJESHA MIKOPO

on

Na. Ahmad Mmow, Kilwa

Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imepanga kuendelea kuvifikisha mahakamani vikundi vya ujasiriamali vilivyoshindwa kurejesha mikopo. Hayo yalibainishwa jana na ofisa maendeleo ya jamii ya halmashauri hiyo, Mustafa Mtu gwe, wakati wa hafla ya uzinduzi wa jukwaa la wanawake wa Kilwa. Linalotambulika kwa jana la Tumaini Jipya la Wanawake Kilwa(TUJIWAKI), uliofanyika jana mjini Kilwa Masoko.

Mtungwe ambaye idara yake inaratibu na kusimamia mikopo hiyo, alisema pamoja na nia njema ya halmashauri hiyo ya kuanzisha mfuko wa maendeleo ya wanawake kwa lengo la kupunguza umasikini kwa jamii katika wilaya hiyo, lakini kunatatizo la vikundi vinavyokopeshwa kushindwa kurejesha mikopo.

Alisema kutokana na hali hiyo, halmashauri hiyo itaendelea kuvifikisha mahakamani vikundi visivyorejesha mikopo. “Mwezi Januari mwaka huu tulivifikisha vikundi 25 vilivyokopeshwa mwaka 2008 hadi 2014, sasa tunakusudia kuvishitaki vikundi vilivyokopeshwa mwaka 2015/2016 ili vikundi vingine vikopeshwe,” alisema Mtungwe.

Alisema kuanzia mwaka 2013/2014 hadi sasa halmashauri hiyo imechangia shilingi, 144.60 milioni. Huku serikali kuu kupitia mfuko wa maendeleo wa wanawake imechangia shilingi 27.30 milioni. Hivyo kufanya jumla ya fedha zilizokopeshwa kwa vikundi vya wanawake wajasiriamali wilayani humo kuwa shilingi 191.905 milioni kwa vikundi 68. Hata hivyo fedha zilizorejeshwa hadi sasa ni shilingi 47.39 milioni tu.

Mtungwe alizitaja baadhi ya sababu zinazochangia vikundi vingine kushindwa kurejesha mikopo ni kufilisika kutokana na kutokuwa na uwezo na utaalamu wa biashara, kutumia mitaji kinyume cha malengo yanayokusudiwa, kuzigawa fedha kwa mwanakikundi mmoja mmoja ili kila mwanakikundi aendeshe shuguli peke yake, kutokuwa na uhakika wa masoko ya bidhaa inayozalishwa na kutaka au kufariki kwa wana vikundi ambao vikundi viligawa fedha kwa kila mwanakikundi.

Aidha ofisa huyo wa idara ya ustawi wa jamii aliitaja baadhi ya mikakati ya halmashauri hiyo katika kuhakikisha vikundi vinarejesha mikopo kwa wakati kuwa ni kutoa mafunzo ya biashara kwa walengwa kabla ya kupewa mikopo, kufuatilia kwa karibu ili kuendelea kuzibaini sababu zinazochangia ucheleweshaji wa marejesho ya mikopo. Ambapo watu waliohama wakiwa na fedha za mikopo, itabidi wadhamini wao warejeshe mikopo hiyo kwamujibu wa mikataba iliyotumika wakati wanakopeshwa.

Kwa upande wake katibu wa jukwaa hilo, Pili Kuliwa alisema kunaumuhimu mkubwa wa kuendelea kutolewa elimu ya ujasiriamali. kwasababu ukosefu wa elimu ndio unaochangia vikundi kufilisika nakushindwa kurejesha fedha ambazo, I get umekata kukopesha vikundi vingine vyenye uhitaji. “Elimu inatolewa kwa kipindi kifupi sana, tena wakati wa kupata mikopo,” alisema Kuliwa.

Nae mwanachama, Mikaela Ngonyani alitoa wito kwa halmashauri ilishirikishe jukwaa hilo katika usimamizi wa mfuko huo ili uweze kusaidia kudai na kukusanya madeni. Uanzishwaji wa jukwaa hilo ni matokeo ya ufadhili mkubwa unaofanywa na shirika la kima taifa la msaada la Action Aid.

Ambalo licha ya kusaidia uanzishaji wa jukwaa hilo, lakini limekamilika msitari wa mbele katika kuchangia kutekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.

_________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you