AFYA

AUDIO :: NAPE AIPA SAA 24 KAMATI KUTOA MAJIBU JUU YA UVAMIZI WA MAKONDA CLOUDS

on

Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo Mh. Nape Mnauye ameipa saa 24 kamati aliyoiunda kumhoji Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda na kuwasilisha taarifa hiyo kwake.

Nape ametoa agizo hilo mapema leo alipotembelea ofisi za Clouds kwa ajili ya kuwapa pole kwa kile kilichofanywa na Mkuu huyo wa mkoa ndani ya ofisi hizo. Pia amesema serikali inalaani kitendo hicho kilichotokea na sasa inasubiri kumsikiliza mkuu huyo alikuwa na sababu gani za kufanya hivyo kabla ya kutolea Maamuzi.

“Sisi kama Serikali tunalaani kilichotokea. Kwenye nchi ambayo imesaini mikataba ya kimataifa ya uhuru wa habari, na nchi yenye Katiba inayolinda vyombo vya habari; hiki kilichotokea ni kunajisi Uhuru wa habari.

Kabla ya kuchukua hatua zozote, sisi kama Serikali tunataka kusikia kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Tumeunda timu ya watu 5 kufanya kazi kwa saa 24 ili wapate maelezo ya Mkuu wa Mkoa. Baada ya hapo tutasema hatua tutakazochukua (kama Serikali) ” – alisema Nape Mnauye

Waziri Nape aliongozana na Mwenyekiti wa Vyombo vya habari nchini Dr. Regnald Mengi na yeye alitoa ya moyoni mwake juu ya kilichotokea. Audio Hii hapa chini Bofya kumsikiliza.

____________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you