AFYA

FEDHA ZA MFUKO WA WANAWAKE KILWA, KIZUNGUMKUTI

on

Na. Ahmad Mmow. Kilwa

Wakati halmashauri ya wilaya ya Kilwa ikiwa katika mikakati ya kuendelea kuvifikisha mahakamani vikundi vya ujasiriamali vilivyoshindwa kurejesha mikopo. Mbunge wa Kilwa kusini, Suleman Bungara, pamoja na kupongeza uamuzi huo ameiinyoshea kidole halmashauri ya wilaya hiyo kushindwa kuendelea kutoa mikopo kwa vikundi vingine vya wanawake wilayani humo.

Bungara maarufu kwa jina la Bwege, aliyasema hayo kufuatia habari iliyoandikwa na Mtandao huu wiki iliyopita. Ambayo ilieleza mikakati ya halmashauri hiyo ya kuhakikisha vikundi vya wanawake ambavyo havijaresha mikopo vinarejesha ili fedha hizo ziweze kukopeshwa vikundi vingine. Ambapo miongoni mwa njia zitakazo tumika ili kufanikiwa lengo hilo ni kuvifikisha mahakamani vikundi hivyo.

Bwege licha ya kuilamu halmashauri hiyo kushindwa kuendelea kutoa mikopo kwa vikundi vingine vya wanawake wilayani humo, lakini pia hakubaliani na kiasi cha shilingi 47.39 milioni kilichorejeshwa na vikundi vya wanawake kuanzia mwaka 2013 hadi 2016. Kwamadai kwamba kiasi kinachotajwa ni kidogo kuliko kilicholipwa.

“Marejesho ya fedha za mfuko wa wanawake ni shilingi 77.86 milioni, hata hivyo fedha zinazorejeshwa hazikopeshwi vikundi vingine. bali zinatumika kwa matumizi mengine,” alisema Bwege.

Bwege ambae ni mjumbe wa kamati ya mikopo ya halmashauri hiyo, aliongeza kusema tatizo la kutopeleka kwenye vikundi fedha zinazorejeshwa limesababisha yeye amfikishie waziri mwenye dhamana ya wanawake ili lipatiwe ufumbuzi. “Waulize katika fedha zilizorejeshwa wamekopesha shilingi ngapi na vikundi vingapi, kuvifikisha mahakamani sawa, lakini waseme fedha wanazo rejesha wanapeleka wapi,” alisema Bwege.

Hivi karibuni kwenye hafla ya uzinduzi wa jukwaa la wanawake wa Kilwa, linalotambulika kwa jina la Tumaini Jipya la Wanawake Kilwa (TUJIWAKI), ofisa wa idara ya maendeleo ya jamii, Mustafa Mtungwe alisema miongoni mwa changamoto zilizopo katika kukopesha mikopo kwa vikundi vya ujasiriamali vya wanawake wilayani humo ni baadhi ya vikundi kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati na kusababisha kushindwa kuvipatia vikundi vingine vilivyopo katika wilaya yenye vikundi 68 vya wanawake wajasiriamali.

Miongoni mwa hatua ambazo halmashauri hiyo itachukua nikuvifikisha mahakamani vikundi visivyorejesha mikopo. Ikiwa nimuendelezo. Kwani mwezi Januari mwaka huu ilifikisha mahakamani vikundi 25. Ofisa huyo alitaja kiasi cha fedha zilizokopeshwa kwa vikundi kuanzia mwaka 2013 hadi 2016 ni shilingi 144.605 milioni. Ambapo kiasi cha fedha zilizorejeshwa katika kipindi hicho ni shilingi 47.39 milioni tu. Huku shilingi 97.21 milioni kikiwa hakijareshwa hadi sasa.

Kwamujibu wa ofisa huyo ambae alimuwakilisha mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo kwenye hafla hiyo nikwamba mwaka 2013 /2014 fedha zilizotolewa ni shilingi 43.15 milioni, 2014/2015 ni 8.66 milioni, 2015/2016 ni 9.84 milioni na mwaka 2016/2017 ni 72.605 milioni. ambapo fedha zilizorejeshwa katika kipindi hicho mwaka na kiasi cha fedha zilizorejeshwa kwenye amana ni 2013/2014(43.15 milioni), 2014/2015(2.46 milioni), 2015/2016(1.77 milioni) na 2016/2017 hakuna fedha zilizorejeshwa.

Juhudi za kumpata mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Zabron Bugingo atoe maoni na maelezo yake kuhusu madai ya mbunge huyo hazikuzaa matunda hadi habari hii inaandikwa. Baada ya simu yake ya mkononi kutokuwa hewani muda wote aliopigiwa na kutumiwa ujumbe mfupi wa simu.

_________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you