AFYA

WAZIRI LWENGE AZISHAURI HALMASHAURI NJIA YA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA MAJI

on

Na. Ahmad Mmow, Kilwa

Halmashauri nchini zimeshauriwa kutenga fedha kwenye bajeti zake ili zitumike kujengea mabwawa ya maji. Ushauri huo umetolewa leo kijijini Mingumbi wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi, na waziri wa maji na umwagiliaji, Gerson Lwenge wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa maji wa Mingumbi-Miteja.

Lwenge alisema wakati serikali kuu ikitimiza wajibu wake wa kupeleka fedha kwenye halmashauri ili zitumike kutekelezea miradi ya maji. Halmashauri kwa upande wake zitenge fedha kutoka kwenye bajeti zake ili zitumike kujengea mabwawa ya maji. Alisema serikali kuu imeendelea kutimiza wajibu wake wa kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama, ikiwamo kutekelezea miradi mkubwa ya maji. Halmashauri zione umuhimu wa kujenga mabwawa katika maeneo yenye uhaba na uhitaji mkubwa wa maji.

Alisema kwa kuzingatia ukweli huo viongozi wa mikoa na wilaya wahakikishe miradi ya maji inapelekwa kwenye vijiji visivyo fikiwa na miradi hiyo.

“serikali imekuwa ikituma fedha mikoani ili zitumike kwa ajili ya miradi ya maji, mkoa wa Lindi ulipewa takribani shilingi 9.00 bilioni. Mpaka sasa zimetumika takribani shilingi 6.00 bilioni, shilingi bilioni tatu hazijatumika.” kwahiyo azisheni miradi kwani fedha zipo, “alisema Lwenge.

Sambamba na wito huo, waziri Lwenge amewataka wakuu wa wilaya kuzifanyia ukaguzi fedha za michango ya watumiaji maji zilizopo kwenye kamati za maji ili zitumiwe na watu wachache kwa masilahi yao binafsi.

Aidha waziri huyo mwenye dhamana ya maji na umwagiliaji amewataka viongozi wa ngazi zote za utawala wasimamie sheria ya mazingira ili kukomesha uharibifu wa mazingira unaosababisha uharibifu wa vyanzo vya maji. Huku akiwataka wananchi kutunza miradi inayojengwa katika maeneo yao. Kwasababu miradi hiyo ni mali yao na ipo kwaajili yao.

Mradi wa Mingumbi – Miteja ulionza kutekelezwa mwaka 2015 na unaotarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu. hadi kukamilika unaotarajiwa kutumia shilingi 4.7 bilioni. Ambapo wakazi 18120 wa vijiji Sita watanufaika.

_______________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you