AFYA

AKAUNTI FEKI YA NAPE NNAUYE YAIBUKA NA KUCHAFUA HALI YA HEWA

on

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ameukanusha ujumbe unfortunate kupitia akaunti ‘feki’ ya twitter yenye jina lake na kuwataka wanaofanya hivyo waache kwani anawafahamu na amesema atawataja.

Nape ameandika hayo leo baada ya akaunti hiyo feki kuandika: “Amemzuia Kinana kuzungumza, akae akijua hakuna marefu yasiyokuwa na ncha”

Akaunti hiyo feki  pia iliandika: “Siyo wote wenye nidhamu ya woga kunyamazia udhalimu unaowafanyia, utawazuia watu kuzungumza hadi lini? Katibu wangu piga moyo konde” Nape alikanusha na kuandika: “Mnahangaika nini kunichafua kwenye twitter, hizi tweet zinazosambwa za maneno yasiyo na busara siyo zangu, nilishasema jana nikamaliza, nitawataja sasa!”
Mbali na hilo Mbunge huyo wa jimbo la Mtama, asubuhi ya leo aliandika ujumbe wa kuwashukuru wanahabari na kusema alikuwa hajui kama wanampenda kiasi kile. Kupitia akaunti yake ya Twitter  “Wanahabari mme GUSA sana moyo wangu!Sikujua kama mnanipenda na kunithamini kiasi KILE!Nawashukuru SANA kwa kujitolea kwenu!Nawapenda SANA!”

FULLVIDEO: Alichokizungumza Nape Nnauye alipokutana na Waandishi wa Habari

________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you