Wasanii

ALICHOKISEMA NAY WA MITEGO MARA BAADA YA KUTOKA SERO

on

Mwanamuziki Nay wa Mitego ameachiwa huru kutoka katika Kituo cha Polisi cha Kati Dar es Salaam ikiwa ni saa chache tangu Rais Dkt Magufuli aliporuhusu kuchezwa redioni kwa wimbo wake uliokuwa umefungiwa na BASATA.
Agizo hilo la Rais Magufuli limetolewa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Mwakyembe alipokuwa akizungumza na waandishi habari mkoani Dodoma.
Waziri Mwakyembe alisema kuwa Rais Magufuli amesema wimbo huo ni mzuri, na kumshauri Nay wa Mitego aongezee mambo mengine kama  kuwataja watu ambao wanakwepa kodi, watumiaji wa dawa za kulevya.
Nay wa Mitego alikamatwa usiku wa kuamkia jana ambapo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Mvomero na baadae alisafirishwa hadi Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam.
Baada ya kutoka, Nay wa Mitego amezungumza na waandishi wa habari na kuwashukuru wale wote waliojitokeza na kumsaidia kwa namna yoyote ile.
Amewashukuru Watanzania wote lakini pia wasanii waliokwenda kumuona na kumtumia jumbe za kumpa moyo, lakini pia mawakili wake waliopambana kwa muda wote kuhakikisha kuwa haki yake inakuwepo na kulindwa.
“Asante kwa wote walioamka na kuwa upande wangu, upande wa haki, walioamini kile ambacho nimekifanya nawashukuru sana”. Amesema Nay wa Mitego

____________________________________________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you