Kitaifa

Madiwani Halmashauri ya Kilwa wagoma Kusoma Taarifa za Kata zao.

on

Na. Ahmad Mmow, Kilwa

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, bila kujali tofauti ya vyama vyao vya siasa. Leo wagoma kusoma taarifa za kata zao kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani la halmashauri hiyo.

Wakiwa katika kikao hicho kilichofanyika leo mjini Kilwa Masoko, madiwani hao waligoma kusoma taarifa za kata zao ikiwa ni agenda ya pili ya kikao hicho kilichokuwa na agenda tatu tu. Kwa madai kuwa wasingeweza kusoma taarifa hizo bila kujua sababu zinazosababisha vikao vya halmashauri hiyo havifanyiki kwa kuzingatia kalenda ya vikao kama kanuni zinavyoeleza.

Diwani wa kwanza kutoa hoja hiyo kwenye kikao hicho cha kawaida cha robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2016/2017, alikuwa Diwani wa kata ya Miteja(CUF), Ibrahim Msati. Diwani Msati alisema kwa mujibu wa kanuni ya 3(1) kulikuwa hakuna haja ya wao kusoma taarifa za kata zao bila ya kujua sababu zinazosababisha kanuni hiyo inayotaka halmashauri au mamlaka za miji kufanya mkutano maramoja kila baada ya miezi mitatu. Kwa kuzingatia kalenda iliyopangwa na halmashauri. Ambayo pia inaonesha tarehe, muda na mahali itapofanyika.

Diwani huyo alisema kikao hicho kilitakiwa kifanyike tangu mwezi Januari mwaka huu. Hata hivyo hakikufanyika. Alisema kutofanyika vikao kwawakati ndiko kunakosababisha halmashauri hiyo kupata hati chafu za ukaguzi. Kwamadai kwamba kunamambo yanayofanywa bila wao kuyajua.

“Waheshimiwa madiwani wenzangu tusikubali kusoma taarifa bila kumjua anaesababisha hali hii, baraza libadilike liwe kamati. Wala hatumlengi mtu yeyote ila tuujue ukweli,” alisema Msati.

Diwani Nassoro Kimbugu wa kata ya Kandawale(CCM), alisema wao kama madiwani wenye nia ya kuwatumikia wananchi waliowachagua walikubali kufanya vikao hata bila posho. Hivyo hakuona sababu ya kutofanyika vikao kwa mujibu wa kalenda iliyopo. Kimbugu alibainisha kwamba hata vikao vya kamati ya fedha na mipango ambavyo vinatakiwa kufanyika kila mwezi havifanyiki.

“Sasa mwezi watatu hazijafanikiwa, lakini matumizi yanafanyika, sisi tupo kisheria ili mambo yaende sawa. Vikao vimenoki(vimeshindwa) baraza liwe kamati tumjue anaekwamisha,” alisema Kimbugu.

Nae diwani wa kata ya Mandawa, Swahaba Matajiri (CUF) alisema hakukuwa na sababu za kusoma taarifa hizo kwasababu baadhi ya changamoto ambazo zingeelezwa na kujadiliwa zimekwisha au zimeshasababisha madhara kutokana na kutoshugulikiwa kwa wakati. Alisema taarifa hizo zinalengo la kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali. Kwahiyo kuna umuhimu mkubwa wa kuzingatia kalenda ya vikao.

Matajiri alishauri taarifa hizo, ambazo, itaendelea kuwa muhimu ziunganishwe na taarifa za kuanzia mwezi Januari ili zisomwe kwenye kikao cha robo ya tatu kitakachofanyika mwezi ujao. Kwasababu taarifa nyingi za nyuma zimepitwa na wakati. Ushauri huo uliungwa mkono na Massa Kinjokwile wa kata ya Kikole(CCM) ambae alisema walikuwa hawezi kusimama nakusoma taarifa ambazo kwa sasa hazina umuhimu tena. Huku akitahadharisha kwamba wapo kwa ajili ya kutetea na kulinda masilahi ya wananchi.

“Kwahiyo tunapouliza tunahitaji majibu sahihi sio majawabu, ndipo tunaona umuhimu wa baraza hili ligeuke kuwa kamati ili tupewe majibu badala ya majawabu, “alisisitiza Kinjokwile.

Akijibu mlalamiko na hoja za madiwani hao, kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, Sylvester Mashema, alisema hakukuwa na uzembe wowote uliosababisha kikao hicho kutofanyika kwa wakati. Bali Kulikuwa na changamoto ambazo hazikuweza kuzuilika. Alizitaja baadhi ya sababu kuwa ni maandalizi ya kikao cha bajeti na muda ambao ungefanyika kikao hicho kujibu hoja za ukaguzi na baadhi ya wakuu wa idara kuwa nje ya halmashauri kwa maslahi ya halmashauri hiyo.

Kaimu mkurugenzi huyo pia aliwakumbusha madiwani hao makubaliano waliyofanya kwenye baraza hilo:“Hata hivyo ilikubaliwa vikao hivi vitaketi baada ya kufanyika vikao vya mamlaka ya miji ya Kilwa Masoko na Kivinje, yote hayo yalichangia,” alisema Mashema.

Hatahivyo, pamoja na majibu hayo baraza hilo kwa kutumia kifungu cha 36 cha kanuni kilibadilika na kuwa kamati. Baada ya kujadili mwenendo mzima wa jambo hilo, kamati hiyo ili rudi ukumbini na uamuzi wa kutosomwa taarifa hizo. Bali zitasomwa katika kikao cha robo ya tatu, hasa taarifa za kuanzia mwezi Januari hadi Machi. Mbali na hayo, mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Abou Massa, alisema kikao kitakacho fanyika kesho kitafanyika iwapo ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo utafungwa feni. Iwapo hazitafungwa ni vigumu kufanyika.

Hivyo amewataka watendaji wa Halmashauri hiyo wanazifunga na kuhakikisha zinaweza kufanya kazi kabla ya kikao hicho kufanyika.

_____________________________________________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you