Wasanii

Harmonize, Idris Sultan kwenye BIFU ZITO

By

on

Moja kati ya kazi zangu ni kuhakikisha haupitwi na chochote ambacho kinajiri katika mitandao ya kijamii. Na katika kulitimiza hilo nimekuletea drama za wakali wenye majina yao hapa Bongo.

Mmoja ni mkali kutoka Usafini WCB Wasafi Harmonize na mwingine ni mshindi wa BBA mwaka 2014 Idris Sultan. Wakali hawa wamezua gumzo kinoma noma katika mitandao ya kijamii baada ya kuonekana wakitupiana vijembe katika mitandao hiyo ya kijamii siku ya jana.

Picha lilianza kwa Idris Sultan ambaye aliamua kupost na kuandika caption iliyosomeka kama “Ogopa rapa wako anapo kiki kuliko wewe. Inabidi mbadilishane wewe ndo uwe rapa #MsinitilieMaanani #Najiongelesha Tu”

Kitu ambacho wakali wa hizi kazi waliichukua caption hiyo kama ilivyo na kuitupa kwa Harmonize, na mwisho wa siku Harmonize akalipokea  vibaya jambo hilo na kuamua kujibu dongo hilo kupitia ukurasa wake wa twitter kama uonavyo hapo juu.

Kisha baada ya masaa kadhaa tukashuhudia tena post ya Idris Sultan iliyoonekana kama ni jibu la tweet ya Harmonize.

Mkusanyiko wa matukio yote hayo nimekuwekea full story kwenye video hiyo hapa chini, Bonyeza play uweze kuisanukia story hiyo mwanzo mpaka mwisho.


JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you