Kitaifa

Wanahabari Nchini Wakumbushwa Kuandika Habari Sahihi bila Kuongeza Maoni yao.

on

Na. Ahmad Mmow. Lindi

Wanahabari nchini wamekumbushwa kutimiza wajibu wao kwa umakini wa kuandika habari sahihi bila kuingiza maoni yao. Wito huo umetolewa na ofisa mawasiliano na uhamasishaji jamii kuhusu utafiti wa viashiria na matokeo ya UKIMWI Tanzania 2016/2017, Mihayo Bupamba, mkutano wa wadau wa utafiti wa viashiria na matokeo ya UKIMWI 2016, uliofanyika leo kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi.

Bupamba alisema wanahabari wanatakiwa kuwa makini katika kusikiliza na kuandika. Kwasababu upotoshaji hata ukiwa mdogo unaharibu maana na kusudio la jambo husika kwa wasomaji. Alisema waandishi wanawajibu wa kuchuja habari za kuandika na kuepuka kuingiza maneno na mawazo yao kwenye habari wanazoandika.

Bila kutaja jina la chombo wala siku ambayo habari hiyo ililipotiwa, ofisa mawasiliano huyo alitolea mfano wa chombo kimoja cha habari kilichoripoti kufanyika kwa utafiti huo. Kwamba kilipotosha umma kwa kuandika utafiti huo utakuwa kwa nchi nzima nyumba kwa nyumba.

Wakati ukweli ni kwamba kuna maeneo maalumu yaliyoteuliwa kufanyiwa utafiti huo. Ambayo ni 525 kwenye Kaya 16000, ambapo wananchi 42000 wanatarajiwa kuhojiwa. “Sisi tumeeleza ukweli wote na kila kitu hapa, tunahitaji takwimu ili kujua hali iliyopo ya jambo husika hapa nchini,” alisisitiza Bupamba.

Aliongeza kusema ushiriki wa waandishi wa habari kwenye matukio mbalimbali, ikiwamo hilo la uzinduzi wa utafiti katika mkoa wa Lindi unatoa fursa ya kupata uelewa mpana wa jambo husika. Hivyo ni rahisi kuandika bila kupotosha ukweli. “Msiandike habari katika mfumo unaoweza kuwatia hofu wasomaji badala ya kuwahamasisha washiriki kikamilifu kwenye jambo linalokusudiwa, habari isiyo tengeneza maswali,” aliongeza kusema Bupamba.

Akizungumzia utafiti huo, alisema utangazia pia uwepo wa viashiria vya usugu dawa, kiwango cha maambukizo ya kaswende na homa ya ini kwa watu wenye umri unaoanzia miaka kami na tano. Alibainisha kwamba tafiti zilizofanyika miaka ya 2003/2004,2007/2008 na 2011 /2012 ziliwahusisha watu wenye umri wa miaka 15 hadi 49 tu. Hata hivyo utafiti wa mwaka huu utawahusisha watu wa rika zote kutoka kwenye kaya zilizo teuliwa. huku akiongeza kusema utafiti huo utahusisha vipimo vingi, tofauti na tafiti zilizowahi kufanyika.

“Takwimu za utafiti zitawasaidia watunga Sera kuandaa mikakati mipya ya UKIMWI inayoendana na ukubwa wa tatizo na kuimarisha mipango ya ufuatiliaji na tathimini kwa miradi inayohusu UKIMWI,” alibainisha.

Bupamba aliwaasa wadau hao kutumia nafasi zao kuwapa ushirikiano watafiti watakaokwenda kwenye maeneo yao na kuwahamasisha wananchi, hasa ambao kaya zao zimeteuliwa washiriki katika utafiti huo.

___________________________________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply