Kitaifa

Basi la LEO lapata Ajali, Abiria 48 Wanusurika Kifo – Lindi.

on

Na. Ahmad Mmow. Lindi

Watu Arobaini na nane waliokuwa wanasafiri na Basi la Leo Luxury Coach, leo wanusurika kifo baada ya Basi hilo kuacha njia na kupinduka. Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi, mrakibu mwandamizi wa polisi, Mohamed Likwata alithibitisha kutokea ajili hiyo.

Kamanda Likwata alisema ajali hiyo imetokea leo saa 6:15 mchana, mtaa wa Mbanja eneo la Mambulu Manispaa ya Lindi. Baada ya Basi hilo aina ya Zhongtong lenye namba za usajili T 471 DDW, mali ya kampuni ya Leo. Lililokuwa linaendeshwa na Ali Kaniki, mkazi wa Kibamba(Dar-es-Salaam) kuacha njia na kupinduka.

Likwata alisema abiria 27 kati ya 48 waliokuwa ndani ya gari hiyo walijeruhiwa. Huku akibainisha wazi kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha kwenye ajili hiyo.

“Chanzo cha ajili hiyo ya Basi lililokuwa linasafiri kutoka Tandahimba mkoani Mtwara kwenda Dar-es-Salaam ni mwendo wa kasi, dereva wa Busi hilo tunamshikilia tukimaliza mahojiano nakukamilisha taratibu atafikishwa mahakamani,” alisema Likwata.

Kwa upande wake kaimu mganga mfawidhi wa hosipitali ya rufaa mkoa wa Lindi (Sokoine), Dkt Emmanuel Bomani alikiri kuwa hosipitali hiyo iliwapokea majeruhi 27, Kati ya hao 21 ni wanaume. Dr Bomani alisema majeruhi 19 walipata michubuko midogo walitibiwa na wameruhusiwa kaondoka. Bali majeruhi nane, wanaume sita na wanawake wawili wamelazwa na wanaendelea kutibiwa.

“Majeruhi wawili, kondokta wa Basi hilo anaetambulika kwa majina ya Hassan Haji mkazi wa Kurasini na Fatuma Mohamed wa Kilwa Kivinje hali zao ni mbaya,” alisema Bomani.

Kaimu mganga mfawidhi huyo alisema kondokta Ali amevunjika mfupa wa paja, mfupa mkubwa wa mkono na taya. Vyote vya upende wa kushoto. Ambapo Fatuma amevunjika kifundo cha mkono wa kushoto na kusagika nyama za mkono wa kulia. Wote wawili wamepoteza fahamu. Bomani aliwataja majeruhi wengine wanaendelea na matibabu hosipitalini hapo, majina yao na mkazi yao kwenye mabano kuwa ni Fatuma Ussi(Mdimba-Newala), Sharifu Mpanga(Mbagala – Dar), Joseph Mazengo (Ng’aherezi-Dodoma) na Shahib Wala (Mdimba – Newala).  Wengine ni Peter Kamandu (Chamwino – Dodoma) na Mwinyi Seifu (Mwandege -Dar-es-Salaam). Bomani majeruhi hao sita hali zao zinaendelea vizuri na wote wametambuliwa na ndugu zao.

______________________________________________________________________

JOIN US IN ALL SOCIAL NETWORK

Dont Miss anything!! Follow us at FacebookTwitter and Instagram for more all Infortainment !! Dont Miss to Join us at Youtube Download our Application PLAYSTORE

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply