Kitaifa

AUDIO: Maalim Seif kukamatwa Muda wowote kwa Uchochezi, asema IGP Mangu

on

Jeshi la polisi limesema muda wowote kuanzia sasa litamkamata na kumfikisha mahakamani Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad kwa tuhuma za Uchochezi anaoufanya visiwani Zanzibar.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Ernest Mangu wakati akihojiwa jana katika kipindi cha Funguka kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Azam.
IGP Mangu amesema awali walimruhusu Maalim Seif Kufanya vikao vya ndani kwa nia njema, lakini baadaye wakagundua anavitumia vikao hivyo kuchochea vitendo viovu hasa kwa maasimu wao wa kisiasa.
“Baada ya vikao vile ndipo tulipoanza kushuhudia vitendo viovu, Mahasimu wa Maalim Seif wakichomewa moto mikarafuu yao, Tulimuita na tulimhoji, jalada lake lipo kwaa DPP na muda wowote kuanzia sasa Tutamfikisha mahakamani” amesema IGP Mangu
Unaweza kumsikiliza kwa kubonyeza Play hapa Chini:-

_____________________________________________________________________

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply