Wasanii

Nay wa Mitego Aandika Ujumbe mzito, Asema Maisha yake yako Hatarini

on

Baada ya Kupata misukusuku ya kukamatwa na Polisi akiwa kwenye show yake ya Kimuziki mjini DODOMA msanii Nay wa Mitego ameandika ujumbe mzito kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akisema kuwa kwa sasa Hali ya Usalama wa Maisha yake uko hatarini.

Nay wa Mitego alikamatwa na Polisi na kufikishwa kituo cha Kati jijini Dar es salaam na kukaa SERO baada ya kudaiwa kutunga wimbo wenye maudhui ya kuikashifu serikali.

Huu ndio ujumbe wa Nay wa Mitego:- “Usalama wa Maisha yangu umekua Mdogo kwasasa, Wana panga kunipoteza ikibidi nisiwepo kabisa kwenye hii Dunia. Nipo tayari kwa chochote wanacho panga kufanya Coz sijajipanga kupambana nao, Mimi ni Mwana Muziki si vingine. Kwa chochote kitachotokea Familia yangu itakua na chakuongea. Siwezi kuhama Nchi wala kukimbia nitafia hapa hapa. Na siko tayari kupindisha Chochote.! Nyie Ndo mtanilinda. Sina Mlinzi na sitarajii kua na mlinzi. OnlyGod??#Wapo #Truth”.


_______________________________________________________________________

IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply