MICHEZO

FoxSports wameripoti Uhamisho wa Zlatan Kujiunga na MLS Umekamilika

on

Staa wa kimataifa wa Sweden ambaye anaichezea Man United ya England Zlatan Ibrahimovic ni wiki kadhaa sasa amekuwa akihusishwa kuelekea kujiunga na LA Galaxy ya Ligi Kuu Marekani, Zlatan hadi sasa ameichezea Man United game 41 na kuifungia goli 26 akitoa assist 9 katika mashindano yote.

Uvumi wa staa huyo kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kwenda kujiunga na LA Galaxy ya Marekani unazidi kuwa mkubwa kutokana na staa huyo kutosema chochote kuhusiana na msimamo wake licha ya kuwa kocha wa Man United Jose Mourinho mwezi uliyopita alisema wanasubiri maamuzi ya Zlatan.Kituo cha TV cha Marekani kinachojihusisha na michezo FoxSports kimeandika stori kupitia ukurasa wake wa instagram foxdeportesVerified imethibitika kuwa Zlatan anakuja kutokea Ulaya huku picha yake inayoaminika ya kutengeneza ikionekana kavaa jezi za LA Galaxy.

Kama taarifa za Zlatan Ibrahimovic zitakuwa  za kweli kuwa ataondoka Man United mwisho wa msimu akiwa kamaliza mkataba wake, itakuwa kadumu na Man United mwaka mmoja tu toka ajiunge mwanzoni mwa msimu huu akitokea Paris Saint Germain ya Ufaransa kama mchezaji huru.

_____________________________________________________________________

IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply