Kitaifa

Kitila Mkumbo ajiuzulu nafasi ya Ushauri wa Chama cha Act-Wazalendo

on

Kufuatia Uteuzi wa Rais Leo Jumanne April 4,2017 kwa Kitila Mkumbo kuwa katibu mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji umempelekea Kitila kujiuzuru nafasi yake ya Ushauri ndani ya Chama cha Act-Wazalendo.

Zitto anasema walifanya mashauriano kama chama ikiwemo Kitila Mkumbo, chama kimepokea uteuzi wa Kitila kuwa katibu mkuu. Uteuzi unaonyesha upinzani kuna watu wenye uwezo, weledi na uzalendo wa kuweza kutumika katika utumishi wa Umma.

Zitto amesema: “Kitila ni mtumishi wa umma kwa sababu ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa hio nafasi aliyopata ni kupanda cheo tu ndani ya utumishi wa umma, ni sawa kama angeteuliwa kuwa Vice Chancellor wa chuo kikuu”.

Kwa nafasi ya katibu mkuu, Ndugu Kitila hawezi kuendelea kuwa mshauri wa chama, nafasi ambayo inamfanya ahudhurie vikao vyote vya chama kuanzia ngazi ya chini mpaka kamati kuu na kamati ya uongozi.

Prof. Kitila ameandika barua ya kujiuzulu ushauri wa chama, nimeipokea barua yake na nimemkubalia kujiuzulu kwake kuanzia Leo. Chama kinamshukuru sana mheshimiwa Kitila kwa wakati wote alichokitumikia chama toka tulipoanza chama hiki alipokuwa mshauri wa chama.

Kaulimbiu yote siku zote ni taifa kwanza, leo na kesho hivyo tunamtakia kila laheri ndugu Kitila katika nafasi hii mpya, wizara ni kubwa na muhimu katika nchi yetu.

Zitto emeongeza: “Kwa hatua hii tumeona Rais ameamua kuunganisha nchi yetu kwa kufanya kazi na watu wote bila kuwabagua kwa itikadi zao za vyama. Watanzania ni wamoja na kauli za kuwagawa zinawaumiza zaidi. Tunaamini katika uteuzi huu, Rais ana nia njema na sisi tumempa baraka zote mwanachama wetu mwanzilishi wa chama kwenda kufanya kazi kwenye nafasi ya juu zaidi ya utumishi wa umma”.

__________________________________________________________________________

IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply