Wasanii

Touchez awacharukia wanaomponda kuhusu Young Dee

on

Prodyuza anayesumbua kwa sasa kwa kuwa na ‘hits’ kali sokoni, Mr T Touchez amejinasibu hana historia ya kutengeneza kazi mbovu hivyo wanaomponda kwa kumsajili ‘Paka rapa’ Young D watulie wasubiri kazi kubwa wanayoipika ndipo waanze kuhukumu.

Akizungumza kwenye eNewz ya EATV Mr. T Touchez amesema baada ya kutangaza kuwa amemsaini msanii huyo maneno yamekuwa mengi na watu wamemponda kuwa hawezi kufanya maajabu makubwa kwa sababu yeye siyo mtu wa kwanza kufanya kazi na msanii huyo.

Touchez ameendelea kujinasibu kuwa yeye ana uwezo mkubwa wa kutengeneza muziki na pia muziki upo ndani ya damu yake na hata muziki atakao mtengenezea msanii huyo utakuwa wa tofauti na watu walio uzoea.

“Kwanza ukiachana na mimi kumsaini D yule msanii ana historia kubwa kimuziki. Mimi hata kabla sijakutana alishawahi kuwa na kazi nzuri sana. Hata nilipoamua kufanya naye project nilijua huyu msanii siyo feki kwa hiyo nawaambia watu wa- relax” Alisema Touchez

Aidha Touchez ameongeza kwamba watanzania waendelee kumuamini kwani umebaki muda mfupi wa kuachia wimbo aliomtengenezea msanii huyo ambao ndiyo utakuwa majibu ya kuwafunga midomo watu wote.

Young D ambaye kwa sasa anatamba na ngoma za Furaha pamoja na Young daddy, amepata usajili kwa Touchez Sound baada ya kutofautiana na menneja wake wa kwanza Max kutoka MDB kwa madai ya msanii huyo kurudi kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

___________________________________________________________________

IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply