Lindiyetu TV

VIDEO :: Mke wa Roma Mkatoliki Aongea Mazito, Kutekwa kwa Mumewe

on

Mke wa Roma Mkatoliki, Nancy ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwae Ivan, amedai yeye pamoja na ndugu zake wameshazunguka kila sehemu bila mafanikio kumtafuta mume wake ambaye ametekwa usiku wa Jumatano hii akiwa Studio za Tongwe Record Masaki jijini Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa habari jioni hii, Nancy amesema mara ya mwisho kuzungumza na Roma ilikuwa jana saa kumi na mbili jioni.“Mimi kama mke wa Roma mara ya mwisho niliwasiliana na mume wangu jana saa kumi na mbili jioni, akaniambia anaelekea Tongwe Records kwajili ya kazi zake za kila siku. Baada ya hapo sikuwa nampata tena kwenye simu lakini nikachukulia ni kawaida tu simu imezima, nimekuja kuamka saa 7 nikapokea simu kutoka kwa rafiki yake akaniambia uko na Roma nikamwambia hapana alikuwa Tongwe, akaniambia kuna taarifa kwenye mitandanao na mimi nikaingia nikakuta hizo taarifa kama walizopata watu wengine,” alisema Nancy.

Nancy amengea mengi bofya Play kumsikiliza hapa:

Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es salaam Kamishna Simon Sirro amesema kuwa wamezipata taarifa hizo na wanazifanyia kazi.

_________________________________________________________________

IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply