Wasanii

Zitto Kabwe, Nay wa Mitego watoa Povu Kutekwa kwa Roma na Moni

on

Rapa Roma Mkatoliki ambaye hivi sasa anafanya vyema na wimbo wake ‘Usimsahau mchizi’  msanii mwenzake na Moni Central Zone wamekamatwa na kupelekwa kusikojulikana na watu wasiojulikana.

Katika taarifa iliyotolewa na msanii Prof. Jay ambaye pia ni mbunge wa Mikumi inasema msanii huyo alikamatwa jana akiwa studio.

Prof. Jay ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa Roma Mkatoliki, Moni Centrozone na kijana mmoja wa kazi walikamatwa jana wakiwa studio za Tongwe Records.

“Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za Tongwe Records majira ya saa moja usiku na wamemchukua Roma, Moni na kijana wa kazi na pia wamechukua computer ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana. Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi” aliandika Prof. Jay


Kitendo cha rapper Roma Mkatoliki na Moni Central Zone kuchukuliwa usiku wa jana (Jumatano) wakati walipokuwa studio ya Tongwe Records na kupelekwa sehemu isiyojulikana, kimewaumiaza wengi. Zitto Kabwe na Nay wa Mitego ni miongoni mwa walioumizwa na tukio hilo.

Wawili hao wamekilaani kitendo hicho kupitia mitandao tofauti tofauti. “Uvamizi wa studio ya Tongwe na kumkamata msanii Roma Mkatoliki ni mwendelezo wa uongozi wa kigangstar na lazima kulaani Kwa nguvu zetu zote,” ameandika Zitto kwenye Twitter yake.

Naye Nay kupitia mtandao wa Instagram ameandika, “Kuvamia Ofisi Za watu, heh.! Kumbe nayo ni Kazi.?! Nina Imani uko salama mwanangu, Kamanda @roma2030 Sina ata chembe ya wasi wasi. #Wapo ✊?✊?.”

Mpaka sasa bado haijafahamika wasanii hao wamekamatwa na nani na kwa kosa gani, na pia bado haijafahamika wamepelekwa wapi.

________________________________________________________________

IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply