Kitaifa

Hospitali Feki Yagundulika Nachingwea, Ikitoa hadi Huduma ya Upasuaji

on

Na. Abdulaziz Video, Nachingwea Lindi.

Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Nachingwea ikiongozwa na mkuu wa wilaya Mhe. Rukia Muwango imemkamata bwana mmoja aliejulikana kwa majina ya Selemani Martin Akiendesha huduma za matibabu bila kibali nyumbani kwake (nyumba ipo mashambani mbali na makazi). Bwana Martin amekamatwa katika msako maalum uliofanywa na kamati ya ulinzi na usalama nyumbani kwake. Huduma alizokua akitoa ni pamoja na upasuaji mkubwa ambapo vifaa tiba vilikutwa na damu na alikutwa mgonjwa mmoja aliekua amefanyiwa upasuaji muda huo ambapo kamati ilimkimbiza hospital ya wilaya.Zimekamatwa pia dawa mbalimbali na vifaa tiba kama visu, mikasi, na vyombo vya kienyeji vilivyotumika kama vifaa tiba.Aidha Kijana mmoja na binti mmoja wanaosemekana ni ndugu zake walikuwa wakimsaidia shughuli hizo ili hali hawana elimu wala mafunzo rasmi ya kitabibu. Upasuaji wa Henia alitoza sh 220,000.00. Bwn Martin anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano na hatua zaidi za kisheria.

_________________________________________________________________

IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply