Wasanii

Askofu Gwajima Atangaza Kumsamehe Diamond Platnumz..Ila Atoa Onyo Hili

on

Ikiwa ni April 9, 2017. Askofu Gwajima aliahidi kuweka wazi mambo ya Diamond Platnumz ambayo watu wengi hawayajui kwakuwa yeye amemuimba katika wimbo wake mpya unaojulikana kama “Acha nikae Kimya”. Lakini amedai kuwa hatofanya hivyo kwa kuwa Diamond kupitia mtandao wa Kijamii wa Instagram Alimuomba Msamaha.

Watu wengi leo walifurika katika kanisa hilo na wengine kutazama Live kupitia Youtube wakitarajia kuwa anafunguka makubwa kuhusu Diamond lakini Karibia na Mwisho wa Mahubiri yake alidai Bibilia inasema mtu akiomba Msamaha Hupashwa Kusamehewa hivyo Hata yeye ameamua Kumsamehe na kumsitiri, lakini ametoa onyo kuwa akiendelea kumchokoza wiki ijayo atafunguka.

Gwajima na Diamond wamekuwa tofauti baada ya Diamond Kumuimba askofu huyo katika wimbo wake uitwao “Niache nikae Kimya”

___________________________________________________________________

IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply