Kitaifa

Mafuriko Yaikumba BUKOBA, Watu waokolewa Kwa Mitumbwi

on

Faustine Ruta, Bukoba – Tanzania
ZAIDI ya watu 70 wameokolewa na Serikali baada ya kukumbwa na mafuliko yaliyotokana na mvua iliyoanza kunyesha kuanzia saa 9 usiku.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo wakati alipo hojiwa na waandishi wa habari katika Kata ya Bakoba mtaa wa nyakanyasi. Kinawilo alisema kuwa nyumba zote zilizoko kandokando ya mto kanoni zote zimeathiliwa na maji kiasi kwamba tumetumia mitumbwi ya uvuvi kuvusha watu.
“Niseme tu mpaka sasa hakuna kifo chochote kile Zaidi ya vitu kuhalibika kwa kulowa maji” alisema kinawilo.

Aidha mkuu wa wilaya alisema kuwa wananchi wachukue tahadhali pindi mvua zinaponyesha tu watoke nje ya nyumba kwa usalama Zaidi.Naye Josefati Bonge mkazi wa Omukigusha alisema kuwa katika nyumba yake hakuna kilichobakia kikiwa kizima kwani nimetoka mimi kama nilivyo na ninamshukuru mungu familia yangu haikuwepo. “Kiukweli kuna kila sababu ya kuhama maeneo kama haya maana nihatali kwa binadamu mfano’ waliokuwa wamelala fofo wanahali gani hivyo kunatakiwa kuchukua hatua mapema ili kuhamia sehemu stahiki” alisema Bonge.

Anitha Mziba mkazi wa Nyakanyasi alisema kuwa yeye katika familia yake hakuna alieumia Zaidi ya vitu vyote vyandani hakuna kilichotoka.
“Yani nimewabeba watoto wangu begani mmoja baada ya mwingine wakati huo mimi maji yakiwa yamenifikia kwenye shingo kwakweli ni hatali” alisema Mziba

___________________________________________________________________

IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply