Kitaifa

Rais Magufuli atupa Jiwe Gizani….”Mimi Ni Dereva Mzuri, Lazima Tufike Tunakokwenda”

on

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amesema watanzania wamuamini kuwa yeye ni dereva Mzuri na lori lake analoliendesha ni lazima lifike salama
Rais Magufuli amesema hayo hii leo wakati akiweka jiwe la Msingi ujenzi wa Reli ya kisasa kutoka DSM – Morogoro eneo la Pugu Jijini Dar Es Salaam
Rais Amesema Dereva mzuri hatakiwi kuangalia wala kusikiliza abiria waliopanda kwenye lori lake wanafanya nini bali anachotakiwa ni kuendesha na kuhakikisha abiria wake wote wanafika salama wanakotakiwa kwenda
“Katika lori wapo watakao angalia nje, wako watakaoimba, wako watakaopiga kelele, lakini wewe kama ni dereva mzuri hutakiwi kuyaangalia hayo, wewe endesha lori lifike unakoenda, na mimi niwahakikishie watanzania mimi ni dereva mzuri, ninajiamini nitafikisha lori la maendeleo kule linakotakiwa kufika” amesema Rais Magufuli

____________________________________________________________________________

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply