MICHEZO

Timu ya Borussia Dortmund yanusurika Kifo Baada ya Basi lao kukumbwa na Mlipuko

on

Milipuko miwili imelikumba basi la timu ya Borussia Dortmund iliyokuwa ikielekea kwenye mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa wa Ulaya dhidi ya Monaco.Akaunti ya Twitter ya timu hiyo imethibitisha tukio hilo lilitokea wakati timu ikitoka kwenye hoteli ya L’Arrivee iliyopo maili mbili tu toka uwanja wa Signal Iduna Park wa mjini Dortmund, Ujerumani.Beki Marc Bartra amejeruhiwa kwenye mlipuko huo na amepelekwa hospitali. Mchezo huo uliokuwa uchezwe usiku wa Jana (tarehe 11-04-2017), umeahirishwa hadi kesho (Leo Tarehe 12-04-2017).Chanzo cha mlipuko huo bado hakijulikani.

__________________________________________________________________________

IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply