MICHEZO

Mbwana Samatta ameamua Kueneza Kiswahili Ulaya Kwa Njia Hii hapa

on

Mtanzania anayecheza soka la kimataifa nchini Ubelgiji Mbwana Samatta ameendelea kueneza utamaduni wake kwa wachezaji wenzake ambao anacheza nao katika Club ya KRC Genk ya nchini humo.

Ikiwa ni baada ya kumalizika kwa mchezo wa usiku wa jana wa michuano ya Europa League ammbapo Genk alikaribishwa nchini Spain na kunoana na club ya Celta Vigo na mchezo kumalizika kwa Celta Vigo kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Samatta alipost katika ukurasa wake wa instagram video ambayo ilimuonyesha akiwa anamfundisha mshambuliaji mwenzake wa KRC Genk Jean Paul Boetius kusoma maneno ya kiswahili.

Kama hujafanikiwa kuiona, cheki hapa chini.

Ni dhahiri kwamba Mbwana Samatta ana mapenzi na Taifa lake, kila la kheri Mbwana Samatta katika kuitangaza Tanzania.

___________________________________________________________________________

IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Leave a Reply