Lindiyetu TV

VIDEO :: Abiria wakwama Masaa Mawili, Ubovu wa Barabara Uvinza – Kigoma

on

Mvua zinazoendelea kunyesha Maeneo mengi ya Nchi zimepelekea kuharibu Baadhi ya Miundombinu ya Barabara hata Makazi ya Watu.

April 16, 2017 Abiria kutoka Mkoa wa Kigoma walikumbwa na Adha ya kuchelewa kuendelea na safari yao ya Kutoka Kigoma kuelekea Dar es Salaam kwa kukwama kwa takriban masaa mawili katika eneo la Uvinza hivyo kupelekea kuharibu ratiba ya safari yao hiyo.

Hiyo ilitokana na mvua iliyonyesha na kuathiri barabara hiyo ambayo kwa sasa ipo katika matengenezo. Kufuatia hali ya Barabara kutokuwa katika hali nzuri kulipelekea malori na Mabasi kuweza kukwama na kuziba barabara hiyo.

Japo baadae waliweza kupata msaada kutoka kwa Mkandarasi ambaye aliweza kuleta Katapila na kuweza kuyavuta malori na mabasi hayo yaliyokuwa yamekwama na kuweza kuendelea na Safari.

Tazama Video hapa ya Tukio zima.


IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply