Wasanii

KIMENUKAA :: Yusuph Mlela Amshushia Matusi Nay wa Mitego

on

Msanii wa filamu nchini Yusuph Mlela amemtusi rapa Nay wa Mitego kwa kile anachodai kuwa msanii huyo anapotosha jamii juu ya maandamano waliofanya baadhi ya wasanii  wa filamu nchini.

Yusuph Mlela ambaye kwenye post yake ameonekana kushindwa kutumia lugha ya staha huku akionesha kutokwa na povu jingi kutokana na mapokeo ya mashabiki wa filamu ambao walio wengi wamekuwa wakiwachana wasanii hao na kuwataka kufanya kazi zenye ubora.

Rapa Nay wa Mitego alisikika akisema kuwa baadhi ya wasanii wa filamu ambao waliandamana ni matahira kwani kitendo cha wao kutaka filamu za nje zizuiliwe hakina tija na mantiki yoyote.

@Naytrueboy wasiopenda kuambiwa Ukweli #wapo ????

A post shared by Dj Kizo (@djkizzoo) on

Kutokana na kauli hiyo, ndipo msanii huyo alipoamua kushusha ujumbe kwa msanii Nay wa Mitego “@naytrueboy wewe jamaa si ulikuwa chocolaa wewe Leo umeyapatia kidogo unasahau kwamba nyuma yako kuna kundi la vijana wanatamani kuwa waigizaji\wanamziki wakubwa….acha kupotosha jamii yetu Kwa sababu zako binafsi… SISi wasanii ATUJAKATAZA MOVIE ZA NJE .. TUNATAKA WANAOZISAMBAZA WAFATE TARATIBU ZA KISHELIA ILI UWIANO WA BIASHARA UWEPO ndio lengo LA maandamano.. so acha kutafuta sifa… nakushangaa kuwa na ufikilivu mdogo kama wewe sio Msanii…tunajua matatizo ya filamu zetu na tunafanyia kazi malekebisho..halaf huwezi kufananisha filamu na mziki…..Kwa sababu unajifanya chizi mbabe.. Wewe si mtoto wa manzese unajifanya unajua kupiga ngumi nataka Round 3 tu za boxing kwenye stage ili Tanzania ijue nani tahiraa nikutie adabu….. This is serous coz we mtoto mdogo tu kwangu dole la kati linakuhusu, kuongea sana tabia za kike wewe si hip hop na unajiamini njoo uwanjani chagua popote pale…..THiS is serous ?@naytrueboy nb:nyie mbuzi mnaosema natafuta kiki Mimi sina nia hiyo kwanza sipendi kuongelewa…kikubwa sipendi dharau coz kila MTU ana haki ya kutetea kazi yake …. Sitaki kupendwa kinafki…pia hamnishangazi eti kutonunua movie zetu coz tunajua bongo movie INA wenyewe sio wewe unayesubiri uikute ishanunuliwa uangalie halafu uponde..hamtuumizi vichwa. aliandika hivyo Yusuph Mlela .


IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply