MICHEZO

Viongozi wa Timu ya Simba Wamfuata Waziri Mwakyembe Dodoma

on

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harison Mwakyembe akizungumza na uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wake Bw. Evans Aveva Mjini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, DODOMA
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe amekutana na uongozi wa klabu ya Simba ukiongozwa na Rais wake Bw. Evans Aveva kwenye Ofisi zake Mjini Dodoma.
Uongozi wa Simba umeitikia wito wa Mhe. Mwakyembe wa kukutana naye na kujadili masuala mbalimbali ya mpira wa Miguu zikiwemo fursa na changamoto katika mabadiliko na maendeleo ya uendeshaji wa timu.
Aidha  Mhe. Mwakyembe  amepokea maoni ya Uongozi wa samba na kushauri kuendelea kutoa ushirikiano na wadau wa mpira wa miguu nchini.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa  na Katibu Mkuu Wizara husika prof Elisante Ole Gabriel, Mkurugenzi wa Michezo Yusufu Omary, Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja, na Msajili wa Vilabu na Vyama nchini.

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply