MICHEZO

EPL, Arsenal vs Leicester Kufungua Pazia Leo

on

Leo Arsenal wanafungua pazia la ligi kuu ya nchini Uingereza kwa msimu wa mwaka 2017/2018 ambapo watacheza dhidi ya bingwa wa msimu wa mwaka juzi Leicester City.Msimu huu Arsenal wanaonekana kupania sana kurudisha heshima kwani achilia mbali wameishinda vita ya kumbakisha Alexis Sanchez bali pia wamemnunua Alexandre Lacazette.

Arsenal wamekuwa wakihangaika sana kuhusu suala la mtu sahihi wa kucheka na nyavu na ujio wa Lacazette unaonekana kama muarobaini wa tatizo hilo, na uwepo wake pamoja na Sanchez unaweza wapa Gunners kitu kipya.

Ushindi katika mechi ya ngao ya hisani dhidi ya Chelsea unawapa Guners kujiamini zaidi hii leo wanapoenda kuikabili Leicester ambao wanaonekana kikosi chao hakijatulia.

Leicester msimu huu nao mambo yanaweza kuendelea kuwa magumu kwao kwani kikosi chao ni kile kile na kochwa wao Craig Shakespare hajafanya usajili wa kutisha zaidi ya kumnunua Kelechi Iheanacho toka City.

Arsenal kuanza kwao mechi katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates kunawapa imani zaidi ya kuanza vyema msimu huu wa ligi na pengine Wenger kujaribu kuwapa Guners kile alichowapa 2004.

Chicharito atashangilia akiifunga United?

Javier Hernandez “Chicharito” ni moja kati ya wachezaji vya mashabiki wa Manchester United na hata alipouzwa na Louis Van Gaal wengi walisikitika sana.

Wikiendi hii Chicharito anarudi Old Trafford lakini safari hii akiwa mpinzani wa Manchester United kwani atakuwa amevaa uzi wa wagonga wa London klabu ya West Ham.

Ni utaratibu wa wachezaji wengi wanapozifunga timu zao za zamani kutoshangilia goli, lakini je kwa Chicharito itakuwaje kama akiifunga Manchester United?

“Ni klabu yangu ya zamani, mashabiki wa zamani na uwanja wa zamani il pia kama nikifunga litakuwa bao langu la kwanza kwa West Ham kwa sasa sijawaza kuhusu kushangilia” alisema Chicharito.

Inaonekana kama vile mshambuliaji huyo amepania kuifunga United kwani amesisitiza kuwa kufunga katika mechi ya kwanza litakuwa jambo zuri sana kwa upande wake. United na West Ham zitapambana siku ya Jumapili katika ufunguzi wa Epl.

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply