MICHEZO

Rais Mpya wa TFF ametangazwa rasmi

on

Kutoka Dodoma katika ukumbi wa St Gasper ulipofanyika mkutano mkuu wa shirikisho la soka Tanzania TFF, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Revocatus Kuuli ametangaza matokeo ya uchaguzi Mkuu wa TFF kwa wajumbe, makamu na Rais wa TFF.

Matokeo ya uchaguzi mkuu wa viongozi wapya wa TFF yametangazwa rasmi mjini Dodoma baada ya zoezi zima la uchaguzi kukamilika.

Rais mpya wa TFF ni Walace Karia ambaye ameshinda kwa kura 95 kati ya 128 za wajumbe waliopiga kura kwenye uchaguzi huo.

Karia amewashinda Iman Madega, Shija Richard, Ally Mayay, Emanuel Kimbe na Fredrick Mwakalebela ambao walikuwa wakiwania nafasi ya urais wa TFF.

Kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa TFF, Karia alikuwa makamu wa Rais chini ya Jamal Malinzi ambapo baadae aliendelea kuiongoza TFF baada ya Malinzi kuwa mahabusu akikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi.

Karia ataongoza shirikisho la soka Tanzania kwa kipindi cha miaka minne kwa mujibu wa katiba ya TFF.

 

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply