MICHEZO

Sergio Aguero Afungua akaunti ya Magoli, City Ikiiadhibu Brighton

on

MANCHESTER CITY inayopewa kipaumbele kutwaa Ubingwa wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, Msimu huu Mpya Leo wameanza kwa ushindi wa Bao 2-0 wakiwa Ugenini kucheza na Timu iliyopanda Daraja Brighton.Bao zote za City zilifungwa Kipindi cha Pili katika Dakika za 70 na 75 Wafungaji wakiwa Sergio Aguero na Dunk aliejifunga mwenyewe.

Kesho zipo Mechi 2 za EPL ambazo zitakamilisha Raundi ya Kwanza na ya awali ni huko Saint James Park kati ya Timu iliyopanda Daraja Newcastle kuikabili Tottenham Hotspur na kisha ni Old Trafford wakati Wenyeji Manchester United wakicheza na West Ham United.VIKOSI VILIVYOANZA: Brighton & Hove Albion (Mfumo 4-4-1-1): Ryan; Bruno, Dunk, Duffy, Suttner; March, Propper, Stephens, Brown; Gross; Hemed.

Akiba: Maenpaa, Huenemeier, Rosenior, Sidwell, Murphy, Knockaert, Murray.

Manchester City (Mfumo 3-1-4-2): Ederson; Kompany, Stones, Otamendi; Fernandinho; Walker, De Bruyne, D Silva, Danilo; Jesus, Aguero.

Akiba: Bravo, Sterling, Mangala, Sane, B Silva, Yaya Toure, Foden.

REFA: Michael Oliver

Matokeo: Ijumaa Agosti 11

Arsenal 4 Leicester City 3

Jumamosi Agosti 12

Watford 3 Liverpool 3

Chelsea 2 Burnley 3

Crystal Palace 0 Huddersfield Town 3

Everton 1 Stoke City 0

Southampton 0 Swansea City 0

West Bromwich Albion 1 AFC Bournemouth 0

Brighton & Hove Albion 0 Manchester City 2

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply