MICHEZO

VIDEO :: Azam dhidi ya Simba magolikipa wa onyesha Uwezo, Shuhudia

on

AZAM FC imeshindwa kutumia vyema fursa ya kucheza nyumbani, baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Simba SC katika mchezo mkali wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo, Simba SC inayofikisha pointi nne sawa na Azam, inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa wastani wa mabao, baada ya Prisons nayo kulazimishwa sare ya 2-2 na Maji Maji ya Songea leo Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Simba ndiyo waliouanza mchezo huo kwa kasi na kiu ya kusaka bao la mapema na katika dakika ya nne tu, mshambuliaji Nicholas Gyan alikaribia kufunga kama si mpira aliopiga kwa kichwa baada ya pasi ya kiungo Muzamil Yassin kuokolewa na kipa wa Azam, Mghana mwenzake, Razack Abalora.

Hadi kipyenga cha mwisho kinapulizwa kuashiria dakika tisini za mchezo na zile za nyongeza za Refarii kumalizika matokeo yalibakia kuwa 0 – 0.


IPAKUE APPLICATION YA LINDIYETU.CO.TZ ILI USIPITWE NA STORY KALI KILA SIKU

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply