MICHEZO

Ajibu Aibeba Yanga dhidi ya Njombe Mji

on

Leo Jumapili ya Septemba 10, 2017. Ligi ya Vodacom Tanzania Bara Imeendelea kwa kuzikutanisha Timu tofauti zinazoshiriki ligi hiyo katika Viwanja Tofauti.Mshambuliaji wa Mabingwa watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga Ibrahim Ajib amefanikiwa kuitoa timu yake kifua mbele baada ya kuifungia bao moja la pekee dhidi ya Njombe Mji FC mchezo ulipigwa katika viunga vya Sabasaba mkoani Njombe.

Yanga Sc ilikuwa ikitupa karata yake ya Pili huko Mjini Njombe kwa kukaribishwa na wenyeji wao Njombe Mji ambapo timu ya wanajangwani wenye maskani yao Kariakoo jijini Dar es Salaam wameweza kuondoka na Point Tatu muhimu na kufikisha jumla ya point 4 katika michezo miwili iliyokwisha cheza hadi hivi sasa huku mchezo wa kwanza walilazimishwa sare dhidi ya Ruvu Shooting.

Bao hilo la Ajib limepatikana kwa mkwaju wa faulo ndani ya dakika 16 za mchezo kipindi cha kwanza na kupelekea mpaka dakika 45 za awali kuisha timu ya Yanga kuwa mbele kwa bao moja.

Pamoja na hayo, timu ya Njombe Mji ilionekana kufanya mashambulizi makali wakati walivyorudi kutoka mapumziko lakini kwa bahati mbaya juhudi zao hazikuweza kuzaa matunda ya aina yeyote kwa siku ya leo.Akizungumza mara baada ya mchezo huo kuisha nahodha wa timu ya Yanga Thabani Kamusoko amesema mechi ya leo kwa upande wao haikuwa rahisi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa waliyokutana nayo huko Njombe.

“Wachezaji wamepambana sana katika mechi ya leo, japokuwa mazingira ya baridi yalitusumbua katika mechi ya leo lakini tunamshukuru Mungu tumefanikiwa kupata pointi tatu”, amesema Kamusoko.

MATOKEO YA MECHI ZA LEO KWA UJUMLA.

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Recommended for you

Leave a Reply